Ban alaani mauaji ya wanajeshi Lebanon katika shambulizi

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema anafuatilia kwa masikitiko makubwa matukio katika eneo la Sidon nchini Lebanon. Bwana Ban amelaani mashambulizi dhidi ya askari wa jeshi la Lebanon, ambalo limesababisha hasara kubwa kwa jeshi hilo. Ametuma risala ya rambi rambi kwa familia za wahanga na kwa serikali ya Lebanon.

Bwana Ban amesisitiza kuwa kila mtu nchini Lebanon anatakiwa kuheshimu mamlaka ya kitaifa na taasisi zilizopo chini ya uongozi wa Rais Sleiman, hususan jeshi la Lebanon, ambalo wajibu wake ni kuwalinda raia wote wa Lebanon.

Amesema jamii ya Kimataifa inasimama imara katika kuunga mkono kwa pamoja uhuru, usalama na utulivu wa Lebanon. Amewakumbusha wote nchini Lebanon kuhusu wajibu wao katika kuepuka mizozo na kuendeleza kanuni za heshima na udugu ili kuulinda umoja wa kitaifa wa Lebanon.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031