Ban aitaka serikali ya Sudan Kusini kujizatiti kuwalinda raia

Kusikiliza /

Wakazi wa Jonglei waliokimbia vurugu

Katika mikutano yake ya ana kwa ana na viongozi wa Afrika mjini Yokohama,
Japan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa Sudan Kusini, Salva kiir Mayardit. Viongozi hao wawili wamezungumza kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya Septemba 27 2012 yalosainiwa kati ya Sudan na Sudan Kusini kuhusu masuala muhimu yalosalia kati ya nchi hizo mbili. Bwana Ban ametoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kuendelea kushirikiana na serikali ya Sudan ili kuendeleza utekelezaji wa makubaliano hayo.
Bwana Ban amesisitizia wasiwasi wa jamii ya kimataifa kuhusu hali ya
kibinadamu inayoendelea kuzorota nchini Sudan Kusini, na kutoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kujizatiti zaidi katika kuwalinda raia, hususan katika jimbo la Jonglei.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031