Baa la nzige latishia uhaba wa chakula Madagascar: FAO

Kusikiliza /

 

Nzige

Nchini Madagascar baa la nzige ambalo udhibiti wake unatia mashaka linaripotiwa kutishia usalama na uhakika wa chakula nchini humo kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kama anavyoripoti Jason Nyakundi.

 (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

FAO inakadiria kuwa ifikapo mwezi Septemba mwaka huu karibu theluthi moja ya taifa laMadagascar  itakuwa imevamiwa na nzige na kuyaweka kwenye hatari karibu maisha ya watu milioni 13 au karibu asilimia 60 ya watu wote wa nchi hiyo.

FAO imefanya hitihada za kuchangisha dola milioni 22  kugharamia hatua za dharura za kukabilina na nzige lakini hata hivyo kampeni hiyo  haijaiungwa mkono kikamilifu ikiwa inakabiliwa na uhaba wa fedha. Mkurugenzi wa FAO Jose Graziano da Solva anasema  kuwa iwapo nzige hao hawatadhibitiwa huenda athari zao zikawa za miaka mingi na pia watakuwa vigumu kuwazuia na kwa gharama ya juu.

Kulingana na tathmini iliyofanywa na FAO ni kuwa maeneo fulani yaMadagascartayari yamepoteza kati ya asilimia 40 na 70 ya mchele na mahindi. FAO inakadiria kuwa huenda karibu tani 630 za chakula zikapotea au karibu asilimia 25 ya mahitaji yote ya nafaka nchiniMadagascarsuala ambalo litaaathiri usalama wa chakula na pato la wengi.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930