Nyumbani » 28/06/2013 Entries posted on “Juni 28th, 2013”

IOM yawasilisha msaada kwa wakimbizi 26,000:Syria

Kusikiliza / IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza kufikisha msaada kwa wakimbizi wa Syria 26,000 familia zinazowahifadhi na familia za Kilebanon zinazorejea huko Kusini mwa Lebanon. Katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa ,msemaji wa IOM Jumbe OmariJumbe anasema mapigano kati ya jeshi la serikali ya Lebanon na [...]

28/06/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Sote tuna wajibu wa kutokomeza adhabu ya kifo: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Tuna wajibu wa kuzuia watu wasio na hatia kuwa wahanga wa ukiukwaji wa haki, hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliyotoa kwenye kikao cha ngazi ya juu mjini New York Marekani kuhusu utokomezaji wa adhabu ya kifo.Bwana Ban amesema njia ya kiungwana zaidi ni kuachana na adhabu hiyo ya [...]

28/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya chanjo ya polio Burundi baada ya tishio kutoka DRC

Kusikiliza / polio1

Serikali ya Burundi  kwa ushirikiano na  shirika la Afya Duniani WHO wameanzisha kampeni kabambe  dhidi ya ugonjwa wa kupooza wa polio. Hii ni baada ya Burundi kujikuta  katika kitisho kikubwa cha kuvamiwa na maradhi hayo baada ya nchi  jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuonyesha dalili za Polio katika maeneo ya  kusini na mashariki [...]

28/06/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuuawa kwa wakimbizi wa ndani wawili Myanmar kwa itia hofu: UNHCR

Kusikiliza / Mama na mwanawe

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatiwa hofu na tukio la ghasia lililofanyika Alhamisi Mashariki mwa jimbo la Myanmar la Rakhine na kusababisha vifo vya wakimbizi wa ndani wawili. Watu wengine sita walijeruhiwa katika tukio hilo wakiwemo watoto wawili. UNHCR imetoa wito wa kufanyika uchunguzi haraka wa tukio hilo.Shirika hilo pia [...]

28/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mfumo mpya waanzishwa kuwezesha nchi kupata takwimu sahihi za misitu: FAO

Kusikiliza / Fao yaanzisha mfumo utakao imarisha juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Shirika la kilimo na chakula duniani, FAO limeanzisha mfumo mpya kwenye mtandao ambamo kwao nchi wanachama zitaweza kutumia kuboresha tathmini zao za ukubwa wa misitu, ujazo wa miti na uwezo wa miti kwenye misitu hiyo kuvuta hewa ya ukaa, kama njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.FAO inasema kuwa kwa kufanya hivyo nchi zitaweza [...]

28/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Zerrougui azuru Syria kunusuru watoto.

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na migogoro ya silaha Bi . Leila Zerrougui anatarajiwa kuzuru nchini Syria na nchi jirani kutathimini madhara kwa watoto kutokana na mgogoro nchini humo. Bi Zerrougui ambaye anatarajiwa kuwasili nchini humo leo kadhalika atazitembela Uturuki na Lebanon ambapo atakutana na familia na watoto walioathiriwa [...]

28/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hadhi ya ukimbizi kwa wanyarwanda kukoma mwisho wa mwezi huu: UNHCR

Kusikiliza / UNHCR

Takribani wanyarwanda 100,000 wanaosihi uhamishoni huenda wakapoteza hadiyaoya ukimbizi ifikapo tarehe 30 mwezi huu kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.  (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)   Wale ambao watatambuliwa kuwa wakimbizi ni wale walioihama nchi kabla ya tarehe 31 mwezi Disemba mwaka 1998. UNHCR inasema [...]

28/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya wakimbizi wa ndani CAR ingali tete: WFP

Kusikiliza / raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limesema hali ya wakimbizi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati bado ni tete, na kwamba hali hii huenda ikaathiri vibaya mno kampeni ya sasa ya kilimo ya mwaka 2013 hadi 2014. Joseph Msami na maelezo zaidi (TAARIFA YA JOSEPH MSAMI) Kwa mujibu wa tathmini ilofanywa baada ya timu [...]

28/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi 10 zajitolea kutokomeza malaria Amerika ya Kati na Karibea

Kusikiliza / Mbu

Nchi kumi za Amerika ya Kati na eneo la Karibea zimejiunga kwenye mkakati wa kikanda unaolenga kutokomeza ugonjwa wa malaria ifikapo mwaka 2020, kwa msaada wa hazina ya kimataifa ya kupiga vita UKIMWI, kifua kikuu na malaria, Global Fund.Haya yametangazwa kwenye mkutano wa kikanda wa mawaziri wa afya kutoka Amerika ya Kati na eneo la [...]

28/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindupindu chaua watu 257 huko Jamhuri ya Kidemokrasia y a Kongo

Kusikiliza / Takriban watu 257 waafa kupitia maambikizi ya kipindupindu,DRC

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC yaelezwa kuwa kipindupindu kimesababisha vifo vya watu 257 kwenye jimbo laKatanga kati ya Elfu Kumi na Mmoja waliopata ugonjwa huo tangu mwanzoni mwa mwaka huu.Taarifa hizo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA kama anavyoripoti Assumpta Massoi.  (RIPOTI YA ASSUMPTA) OCHA [...]

28/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM imeanza kufikisha msaada kwa wakimbizi wa Syria waioko Lebanon

Kusikiliza / Wakimbizi wasyria

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza kufikisha msaada kwa wakimbizi wa Syria 26,000 familia zinazowahifadhi na familia za Kilebanon zinazorejea huko Kusini mwa Lebanon.Operesheni za IOM zilisitishwa kwa muda mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na mapigano ya Jumapili kati ya jeshi la serikali ya Lebanon na waasi wanaomuunga mkono kiongozi wa kidini Salafi , [...]

28/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR kusaidia wakimbizi wa Mali kupiga kura ugenini

Kusikiliza / Wakimbizi wa Mali

Ukiwa umesalia mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais nchiniMalihapo Julai 28, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linaimarisha shughuli za kusaidia nchi jirani kukabiliana na upigaji kura wa wakimbizi waMalikatika nchi hizo.Burkina Faso, Niger na Mauritania kwa pamoja zinahifadhi wakimbizi 175,000 waMaliwaliongia kutokana na machafuko ya karibuni. Wakimbizi watakaoweza kupiga [...]

28/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031