Nyumbani » 27/06/2013 Entries posted on “Juni 27th, 2013”

Baraza la Usalama laondoa vikwazo dhidi ya Iraq, laongeza muda wa UNDOF

Kusikiliza / Hoshyar Zebari

Baraza la Usalama leo kwa kauli moja limepitisha azimio la kuiondolea nchi ya Iraq vikwazo vyote ilivyowekewa kutokana na uvamizi wake kwa taifa la Kuwait mwaka wa 1990 na madai ya kuwa na silaha za nyuklia na za kemikali. Vikwazo dhidi ya Iraq viliwekwa mnamo mwaka 1991, wakati wa uongozi wa Saddam Hussein. Baraza hilo [...]

27/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNICEF na washirika kutokomeza utapiamplo Burundi

Kusikiliza / Utapiamlo kutokomezwa Burundi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikina an serikali ya Burundi na washirika wengine wa afya wanajitahidi kupambana na utapiamlo sugu na unyafunzi nchini Burundi. Ungana na Joseph Msami katika makala inayoelezea namna juhudi hizo zinazotiwa shime na UNICEF ,zinavyochukua kasi, katika taifa hilo lililowahi kukumbwa na mapigano miaka ya hivi [...]

27/06/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO NA UNICEF zaitaka DRC ichunguze ubakaji wa watoto

Kusikiliza / Askari wa MONUSCO wawasaidia wanawake na wasichana

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC, Roger Meece na Mkuu wa Shirika la Kuwasaidia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, nchini humo, Barbara Bentine, wameelezea kusikitishwa kwao na matukio ya hivi karibuni ya ubakaji wa wasichana wadogo katika maeneo ya Kavumbu na Ruwiro katika mkoa wa [...]

27/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Amani yaimarika maradufu Liberia:UNMIL

Kusikiliza / Kamanda wa UNMIL Meja Jenerali Leonard Muriuki Ngondi

Wakati makamanda wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa wakiwa wanakutana mjini New York kuwasilisha ripoti zao kuhusu hali ya amani katika nchi husika, mkuu wa kikosi ujumbe wa UM nchini Liberia UNMIL Leonard Kingondi amesema hali ya amani imeimarika nchini humo . Ungana na Joseph Msami

27/06/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Haki za binadamu njia panda wakati machafuko yakishika kasi Iraq

Kusikiliza / Martin kobler

Licha ya baadhi ya hatua kupigwa , haki za binadamu nchini Iraq ziko katika tishio kubwa kutokana na ongezeko la machafuko , imesema ripoti ya haki za binadamu iliyotolewa leo. George Njogopa na ripoti kamili.(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)  Ripoti hiyo iliyochapishwa na ofisi ya tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa kwa [...]

27/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ripoti mpya yaonyesha ukuaji wa uwekezaji wa kigeni katika nchi maskini

Kusikiliza / Ripoti iliyotolewa, UNCTAD

Ripoti mpya ya uwekezaji duniani mwaka 2013 inaonyesha kuwa uwekezaji wa moja kwa moja uliofanywa na wawekezaji wa kigeni katika nchi maskini, (FDI) uliongezeka kwa asilimia 20 mwaka 2012, na kufikia rekodi mpya ya dola bilioni 26.Ripoti hiyo ya kila mwaka ya uwekezaji uitwao Greenfield Investment, na ambayo imetolewa na Kamati ya Biashara na Maendeleo [...]

27/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msaidizi wa Katibu Mkuu Feltman azuru Mogadishu kufuatia shambulizi

Kusikiliza / Feltman

Mkuu wa masuala ya kisiasa katika Umoja wa Mataifa, Jeffrey Feltman, amefanya ziara nchini Somalia leo kufuatia shambulizi la hivi karibuni kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa, UNSOM, na kusisitiza uungaji mkono wa dhati wa Umoja wa Mataifa kwa serikali ya Somalia na watu wake. Shambulizi la tarehe 19 Juni kwenye ofisi za Umoja wa [...]

27/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miaka 20 baada ya makubaliano ya Vienna bado ukatili waendelea: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay-Vienna

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema licha ya mafanikio makubwa  tangu kuanza kutekelezwa kwa makubaliano kuhusu haki za binadamu mjini Viennamwaka 1993, bado makubaliano hayo yamekabiliwa na changamoto nyingi. Grace Kaneiya na ripoti zaidi. (Taariaf ya grace) Akifungua mkutano wa siku mbili hukoAustria wa kuadhimisha miaka 20 tangu [...]

27/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wanaofanya kazi katika sekta ya uvuvi walindwe:FAO/ ILO

Kusikiliza / Watoto wavuvi

Serikali zimetakiwa kuchukua hatua madhubuti za kuwalinda watoto kutokana na madhara ya kazi katika sekta za uvuvi na ufugaji wa viumbe vya majini . Kauli hiyo imetolewa na shirika la kilimo na chakula FAO na lile la kazi ILO. Jason Nyakundi na taarifa zaidi(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Watoto wengi wanapitia hali ngumu  ya kufanya kazi [...]

27/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Akizungumzia kuchanuka kwa Afrika Ban pia akumbuka afya ya Mandela

Kusikiliza / Nelson Mandela, (picha ya maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mmoja wa majabali ya Afrika kwa karne ya 20 Mzee Nelson Mandela yu mahututi hospitali na kusema kuwa mawazo na sala za kila mmoja zinaelekezwa kwake, familia yake, watu wa Afrika ya Kusini na dunia nzima ambao wameguswa na ujasiri na maisha yake. Flora Nducha anaripoti(RIPOTI [...]

27/06/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UNECE yapitisha mipango mipya

Kusikiliza / Gari inayotumia umeme

Shirika la Umoja wa Mataifa la UNECE limefaulu kupitisha agenda muhimu ambayo inatoa mwongozo na kanuni ya usafi wa hydrogen na mitambo inayotumia nishati za kati. Miongozo hiyo inaainisha mambo yanayopaswa kuzingatiwa ili ikiepusha athari zinazoweza kujitokeza wakati kunapofanyika shughuli zikiwemo zile zinazotumia umeme. Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa kupitishwa kwa azimio hilo [...]

27/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msimu wa kiangazi waleta furaha kwa watoto wa kipalestina: UNRWA-EU

Kusikiliza / Watoto

Kwa mwaka wa tatu mfululizo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya, EU wamekuwa wakihakikisha msimu wa kiangazi unakuwa wa furaha kwa watoto wakimbizi wa Kipalestina wapatao Elfu Sita kwenye Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan. Katika kipindi cha takribani cha kuanzia tarehe 23 Juni [...]

27/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930