Nyumbani » 26/06/2013 Entries posted on “Juni 26th, 2013”

UN Women yazindua wito wa kuhakikisha usawa wa kijinsia unafanikiwa

Kusikiliza / UN-Women yazindua wito wa usawa wa kijinsia

Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachiohusika na masuala ya wanawake UN-Women kimezindua wito maalumu wa kimataifa kuhakikisha sababu zinazokwamisha mafanikio ya usawa wa kijinsia , haki za wanawake na kuwawezesha wanawake zinatokomezwa kwa kuchukuliwa hatua madhubuti ambazo zitawawezesha wanawake na wasichana waishii kama raia sawa na wengine popote.Katika waraka uliotolewa leo UN-Women inatoa mwongozo kuhusu [...]

26/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tuwezeshe ujasiriamali kwa vijana ili kubuni nafasi za kazi: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Rais wa Baraza Kuu Vuk Jeremic kwenye kikao kuhusu Ujasiriamali na Maendeleo

Wakati vijana zaidi ya milioni 70 wakiwa hawana ajira, ujasiriamali unaweza kuwa suluhu la kuwabadilisha vijana hao wasio na ajira na kuwafanya kuwa watoaji ajira wakubwa. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, katika hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja huo wakati likukutana kujadili ujasiriamali kwa maendeleo. Bwana Ban amesema kati [...]

26/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa UM aitaka Nigeria kusitisha unyongaji

Kusikiliza / Mauaji

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa dhidi ya mauji ya kiholela na unyongaji bwana Christof Heyns amelaani vikali unyongaji wa watu wane unaodaiwa kufanyika Juni 24 kwenye jimbo la Edo huko Nigeria. George Njogopa na taarifa kamili.  (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)  Bwana Heyns pia ametoa mwito wa kusitishwa utekelezaji wa adhabu ya kunyongwa inayowasubiri watu [...]

26/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Abdallah Wafy kama mwakilishi wake maalum DRC

Kusikiliza / Mwakilishi mpya wa Ban DRC ateuliwa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Bwana Abdallah Wafy kuwa Mwakilishi wake maalumu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako pia atasimamia idara ya uongozi wa kisheria katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo, MONUSCO.Bwana Wafy ambaye amekuwa akihudumu kama Naibu Mwakilishi Maalum kuhusu uongozi wa kisheria katika [...]

26/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

"Sober House" zaokoa vijana waliotumbukia kwenye madawa ya kulevya Zanzibar

Kusikiliza / Madawa ya kulevya, Zanzibar

Ikiwa leo ni siku ya kupiga vita matumizi na usafirishaji wa madawa ya kulevya, huko Tanzania Zanzibar, yaelezwa kuwa vijana waliotumbukia katika matumizi ya madawa ya kulevya wanapatiwa misaada na makazi maalum ya kuwarekebisha tabia zao yajulikanayo kwa kiingerezakamaSober House.Mmoja wa wamiliki wa makazi hayo Bi. Fatma Musa Juma alizungumza na Stella Vuzo wa Kituo [...]

26/06/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi Uganda.

Kusikiliza / Bokova, UNESCO ashtumu mauaji ya mwanahabari, Uganda

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bukova ameitaka mamlaka nchini Uganda, kuendesha uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari Thomas Pere ambaye mwili wake ulikutwa nje kidogo ya mji wa Kampla June 17 mwaka huu. Katika taarifa yake aliyoitoa mjini Paris Ufaransa, Bi [...]

26/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baa la nzige latishia uhaba wa chakula Madagascar: FAO

Kusikiliza / Nzige

  Nchini Madagascar baa la nzige ambalo udhibiti wake unatia mashaka linaripotiwa kutishia usalama na uhakika wa chakula nchini humo kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kama anavyoripoti Jason Nyakundi.  (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)   FAO inakadiria kuwa ifikapo mwezi Septemba mwaka huu karibu theluthi moja ya taifa laMadagascar  itakuwa imevamiwa [...]

26/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa zamulikwa

Kusikiliza / Makamanda wa vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Mataifa wakihutubia kikao cha Baraza la Usalama

MjiniNew York, Marekani hii leo Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepokea taarifa za utendaji wa vikosi vya ulinzi wa amani vya umoja huo, zikiwasilishwa na makamanda wa vikosi hivyo ambao wamekuwa wakikutana hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Joshua Mmali na ripoti kamili. (TAARIFA YA JOSHUA MMALI) Mada kuu ambazo zimejadiliwa [...]

26/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi mpya Burkina Faso kuwezesha nchi hiyo kukabiliana na utapiamlo

Kusikiliza / Utapiamlo ni tishio Burkina Faso, WFP

Kufuatia uhaba wa chakula hukoBurkina Fasomwaka 2012, shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP nchini humo limeanzisha mradi mpya wa kuchagiza jamii kuibuka katika mgogoro huo wa chakula na hatimaye kuweza kukabiliana na halikamahiyo baadaye iwapo itatokea huku pia ikipunguza utapiamlo. Ripoti ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi.(TAARIFA YA GRACE KANEIYA) Burkina Fasoimeshuhudia [...]

26/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi wanachama zatakiwa kutekeleza mkataba wa kupinga utesaji:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuongeza juhudi za kuwasaidia waathirika wa utesaji na unyama wa aina nyingine, vitendo visivyo vya kiutu na adhabu za kudhalilisha. Amesema wakati dunia ikiadhimisha siku ya kuunga mkono waathirika wa utesaji ni muhimu kuimarisha mtazamo unaowagusa waathirika na unaojumuisha masuala [...]

26/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ibua mbinu kuboresha afya na si kubuni dawa mpya za kulevya: UNODC

Kusikiliza / Ujumbe katika kuadhimisha siku ya leo

Fanya afya kipaumbele chako na siyo madawa ya kulevya, ni ujumbe mahsusi wa Umoja wa Mataifa hii leo ambayo ni siku ya kimataifa dhidi ya matumizi na usafirishaji wa madawa ya kulevya. Ripoti ya Flora Nducha inafafanua zaidi.(Ripoti ya Flora) Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti madawa ya kulevya na uhalifu UNODC inaeleza bayana [...]

26/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa UM wazitaka serikali kuwasaidia wahanga wa utesaji na familia zao:

Kusikiliza / Mhanga wa utesaji, apokea matibabu

Serikali zimeaswa kuwa ni lazima zijitahidi kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha kwamba wahanga wa utesaji na familia zao wanapata msaada na unaostahili kutokana na madhila waliyotapata . Kauli hiyo imetolewa na wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuwaunga mkono waathirika wa utesaji ambayo kila [...]

26/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakutana Cairo kujadilia mpango wa kuendeleza nchi za Kiarabu

Kusikiliza / Dr.Babatunde Osotimehin

Viongozi wa kiserikali, mashirika ya kiraia pamoja na wataalamu kutoka sehemu mbalimbali duniani wamerejea tena Cairo nchini Misri, kwa ajili ya kutathmini mpango ulisisiwa nchini humo mnamo mwaka 1994 ambao uliweka maazimio yanayohusu idadi ya watu kwa nchi za kiarabu na agenda ya maendeleo kuelekea mwaka 2014. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la [...]

26/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031