Nyumbani » 25/06/2013 Entries posted on “Juni 25th, 2013”

Baraza la Usalama lajadili hali Mashariki ya Kati

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limekutana na kushauriana kuhusu hali ya usalama Mashariki ya Kati, ukiwemo mizozo ya Syria, na suala la Palestina. Katika mkutano huo, Naibu wa Mkuu wa masuala ya Kisiasa katika Umoja wa Mataifa, Fernandez Taranco, ameliambia Baraza la Usalama kuwa hali katika Mashariki ya Kati inaufanya sasa kuwa wakati [...]

25/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watunga sera warahisishe uhamiaji na si kuzuia: UM waelezwa

Kusikiliza / wahamiaji waliokamatwa Morocco

Uhamiaji ulikuwepo na utaendelea kuwepo na una nafasi kubwa katika maendeleo ya nchi yoyote ile duniani hivyo ni wajibu wa watunga sera kuweka mazingira ya kurahisisha uhamiaji badala ya kuweka vizingiti. Hiyo ilikuwa sehemu ya kauli ya Douglas Massey kutoka Chuo Kikuu cha Pricetown kwenye kikao cha ngazi ya juu cha Umoja wa Mataifa mjiniNew [...]

25/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria inakwaza ajira za mabaharia: Nahodha Mlesa

Kusikiliza / Siku ya mabaharia duniani

Ikiwa Juni 25 ni siku ya kimataifa ya mabaharia, Umoja wa Mataifa umezungumzia umuhimu wa zaidi ya mabaharia Milioni Moja na nusu duniani kote ambao huwezesha kusafiri salama kwa shehena mbali mbali baina ya mabara, nchi na maeneo. Hata hivyo mabaharia hao hukumbwa na mikasakamavile uharamia, vimbunga na kadhalika ali mradi misukosuko baharini. Na zaidi [...]

25/06/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban apongeza jukumu la mabaharia katika kuchagiza biashara ya kimataifa

Kusikiliza / Siku ya mabaharia duniani

Leo ni siku ya mabaharia duniani ambapo Umoja wa Mataifa umetaka kuchagizwa kwa harakati za kuongeza idadi yao kwa mustakhbali wa biashara bora duniani. Alice Kariuki na taarifa zaidi. (ALICE TAARIFA) Bila mchango wa mabaharia milioni 1.5 duniani , biashara ya kimataifa itakuwa katika hatihati amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Katika [...]

25/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili hali nchini Mali

Kusikiliza / Mali Kaskazini

  Kwa mara nyingine tena, hali nchini Mali imekuwa suala la kuangaziwa katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Joshua Mmali amekuwa akiufuatilia mkutano huo. (TAARIFA YA JOSHUA MMALI) Mkutano wa leo wa Baraza la Usalama, umehudhuriwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu kuhusu eneo la Sahel, Romano Prodi, Waziri wa Mambo ya [...]

25/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utapiamlo waigharimu Ethiopia asilimia 16.5 ya pato lake la kitaifa

Kusikiliza / Mtoto mwenye utapiamlo Ethiopia akichukuliwa vipimo

Taifa la Ethiopia linapoteza karibu asilimia 16.5 ya pato lake la kitaifa kutokana na athari za muda zinazotokana na utapiamlo miongoni mwa watoto kwa mujibu wa Shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Hii ni moja ya takwimu zinazochipuza kutokana na utafiti wenye kichwa "Gharama ya Njaa barani Afrika" kuonyesha athari za utapiamlo kwenye mataifa [...]

25/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi saba barani Afrika zapunguza maambukizi ya Ukimwi kwa watoto: UNAIDS

Kusikiliza / Mama anayeishi na virusi vya Ukimwi akiwa na mwanae nchini Namibia

Ripoti mpya kuhusu mipango ya kimataifa ya kupunguza na kumaliza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watoto ifikapo mwaka 2015 na kuwaongozea maisha mama zao imeonyesha hatua zilizopigwa katika kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watoto barani Afrika . Assumpta massoi anaripoti.  (RIPOTI YA ASSUMPTA MASSOI)   Ripoti hiyo inaonyesha kuwa [...]

25/06/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

IOM na Tunisia zachapisha utafiti mpya kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu

Jumbe Omari Jumbe

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM limechapisha utafiti wake unaoangazia hali usafirishaji haramu wa watu nchiniTunisia. Utafiti huo ambao umefanywa kwa pamoja kati ya IOM na serikali ya Tunisia unaonyesha kuwa vijana wengi nchini humo wapo hatarini kusafirishwa katika mataifa ya nje. Waendeshaji wa vitendo hivyo wanaripotiwa kutoa ahadi za uongo kwa vijana hao ikiwemo [...]

25/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali mbaya Syria yaondoa matumaini ya mazungumzo ya amani:

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Umoja wa Mataifa, Urusi na Marekani wanakutana mjini Geneva kwa duru ya pili ya mazungumzo ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa kuhusu Syria. Akizungumza kabla ya mkutano wao mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Syria Lakhdar Brahimi amesema hali nchini Syria inazidi kuzorota na mipango ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa kuhusu Syria [...]

25/06/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031