Nyumbani » 24/06/2013 Entries posted on “Juni 24th, 2013”

Ban alaani mauaji ya wanajeshi Lebanon katika shambulizi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema anafuatilia kwa masikitiko makubwa matukio katika eneo la Sidon nchini Lebanon. Bwana Ban amelaani mashambulizi dhidi ya askari wa jeshi la Lebanon, ambalo limesababisha hasara kubwa kwa jeshi hilo. Ametuma risala ya rambi rambi kwa familia za wahanga na kwa serikali ya Lebanon. Bwana Ban amesisitiza [...]

24/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watekelezaji wa ukatili wa kingono sasa kukiona cha mtema kuni: UM

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama la UM

Hatimaye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limechukua hatua thabiti kuhakikisha kuwa watekelezaji wote wa vitendo vya ukatili wa kingono kwenye maeneo ya mizozo wanakumbana na mkono wa sheria. Na hii imekuja baada ya barazahilokupitisha azimio jipya ambamo kwalo linaimarisha juhudi za kuepusha watuhumiwa kukwepa mkono wa sheria wanapofanya vitendo hivyo siyo tu kwa [...]

24/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafuriko nchini India, Ban atuma salamu za rambirambi kwa wafiwa

Kusikiliza / Athari za mafuriko nchini India

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameelezea majonzi yake kutokana na vifo, uharibifu wa makazi na miundombinu nchiniIndiakulikosababishwa na mafuriko kwenye jimbo la Kaskazini la Uttarakhand wiki iliyopita. Msemaji wa Bwana Ban amemkariri Katibu Mkuu akituma rambirambi kwa serikali yaIndia, wafiwa na pole kwa majeruhi na walioathirika kwa namna moja au nyingine na [...]

24/06/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mji wa Kaesong nchini Korea Kaskazini watajwa kuwa mji wa kihistoria

Kusikiliza / Sanamu ya Kim-iL-Sung, mjini Kaesong

Mji wa kihistoria waKaesong ulio nchini Korea Kaskazini  umetamngazwa kuwa mji wa kihistoria  wakati Umoja wa Mataifa unopoendelea kutathimini maajabu ya kiasili na kitamaduni kote duniani.Kamati ya masuala ya kitamaduni kwenye shirika la elimu , sayansi na utamabudini la Umoja wa Mataifa UNESCO hii leo iliidhinisha mji huo kwenye mkutano unaondelea nchiniCambodiakutokana na umuhimu wake kwenye [...]

24/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laangazia ukatili wa kingono kwenye migogoro

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza william Hague kwenye kikao.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na mjadala kuhusu ukatili wa kingono kwenye migogro hususan kitendo cha watuhumiwa kukwepa mkono wa sheria huku wanawake na watoto wa kike wakikabiliwa na msongo baada ya kufanyiwa vitendo hivyo. Joshua Mmali alifuatilia mjadala huo na hii hapa ni taarifa yake. (PKG YA JOSHUA MMALI

24/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto ndio wajenzi na viashiria vya jamii zenye afya na endelevu: UNICEF

Kusikiliza / Watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema mwaka mmoja baada ya mkutano wa Rio+20 kuhusu mustakhbali tunaohitaji, ni dhahiri shahiri kuwa matokeo ya mkutano huo yatategema vile ambavyo watoto watawekwa kuwa kitovu cha ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. George Njogopa na taarifa zaidi. (RIPOTI YA GEORGE) UNICEF katika taarifa yake hiyo [...]

24/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano kuhusu hatma ya miji waanza huko Sweden

Kusikiliza / CITIES

Huko Stockholm, Sweden wasomi, wataalamu wa makazim, watunga sera na wahusika wa maeneo ya umma wanakutana ili kujadili hatma ya maeneo hayo wakati huu ambapo ukuaji wa miji unashindwa kwenda sambamba na utoaji huduma za msingi kwa wakazi wake. Mkutano huo umendaliwa na shirika la makazi ya watu la Umoja wa Mataifa, UN-HABITAT kama anavyoripoti [...]

24/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yasema chakula na lishe bora ni kipaumbele kwa Paksitani

Kusikiliza / Ertharin Cousin

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, Ertharin Cousin amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Pakistani ambapo ametaka jitihada mpya za kushughulikia suala la chakula na lishe nchini humo miongoni mwa watu wanaokabiliwa na ukimbizi wa ndani, majanga ya asili na umaskini. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi. (Taarifa ya Assumpta) [...]

24/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha hatua ya Albania kuwapatia makazi raia wa Iraq

Kusikiliza / Martin Kobler

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amekaribisha hatua ya kupewa makazi upya huko Albania kwa raia 27 wa Iraq waliokuwa wakiishi katika kambi moja iliyoko karibu na mji wa Baghdad.Hadi sasa kiasi cha watu 71 wanaarifiwa kuwasili salama huko Albania na tayari wameenza kunufaika na misaada inayoendelewa kutolewa na serikali [...]

24/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na shambulio dhidi ya watalii huko Pakistani

Kusikiliza / Katibu Mkuu, Ban Ki-moon

Ripoti ya kwamba kundi la wapanda mlima wa kigeni walishambuliwa na kuuawa huko Kaskazini mwa Pakistani zimemsikitisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye pamoja na kutuma salamu za rambi rambi kwa wafiwa, ameonyesha wasiwasi wake juu ya ongezeko la mashambulio ya kigaidi nchini humo.Bwana Ban amesema katika wiki chache zilizopita pekee, makumi [...]

24/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031