Nyumbani » 21/06/2013 Entries posted on “Juni 21st, 2013”

Lugha ya Kiswahili yazidi kuenea kwenye medani za kimataifa

Kusikiliza / Uzinduzi wa muhtasari wa ripoti ya maendeleo ya binadamu katika lugha ya Kiswahili mjini New York

  Kwa mara ya kwanza ripoti ya Maendeleo ya binadamu inayoandaliaw na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa imekuwa na muhtasari wake katika lugha ya Kiswahili. Uzinduzi wa muhtasari huo ulifanyika Kilifi, Mombasa Kenya tarehe 12 mwezi huu wa Juni na siku ya Alhamisi ya tarehe 20 Juni mjini New York Marekani, [...]

21/06/2013 | Jamii: Makala za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji wa haki za binadamau bado tishio Sudan:UM

Kusikiliza / Mashood Baderin

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Sudan Mashood Baderin amesema licha ya hali ya haki za binadamu kuimaraika nchini humo , bado kuna changamoto ya ukiukwaji wa haki hizo katika baadhi ya sehemu. Akitoa ripoti ya ziara yake ya tatu nchini humo, mtaalamu huyo amesema leo mjini Geneva kuwa jumuiya [...]

21/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lugha ya Kiswahili yazidi kung'ara medani za kimataifa: Balozi Kamau

Kusikiliza / Balozi wa Burundi, Tanzani na Kenya (kushoto-kulia)

Baada ya kuzinduliwa huko Kilifi, Kenya wiki iliyopita, muhtasari wa ripoti ya Maendeleo ya binadamu kwa mwaka 2013 katika lugha ya Kiswahili iliwasilishwa rasmi mjini New York, Marekani na kushuhudiwa na wageni mbali mbali ikiwemo wawakilishi wa nchi za Angola, Burundi, Uganda, Tanzania na Kenya na Umoja wa Afrika katika Umoja wa mataifa.Ripoti hiyo inayoonyesha [...]

21/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA yalaani mauaji ya wakimbizi sita wa kipalestina huko Damascus

Kusikiliza / UNRWA yalaani mauaji ya wakimbizi wakipalestina

Masahibu yanayokumba wakimbizi wa Syria ni zaidi ya uhaba wa chakula ambapo ripoti zinasema kuwa wakimbizi sita wa kipalestina wameuawa  nje kidogo ya mji mkuu waSyria,Damascus baada ya makombora yapatayo matatu kutua katika kambi ya wakimbizi wa kipalestina ya Khan Eshieh. Hadi sasa haijafahamika nani aliyerusha makombora hayo. George Njogopa na maelezo zaidi.(RIPOTI YA GEORGE [...]

21/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka Libya isaidiwe kuimarisha mifumo ya usalama na sheria

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limetoa wito kwa jamii ya kimataifa iendelee kuisaidia serikali ya Libya katika juhudi zake za kuongeza uwezo wa taasisi zake za kiusalama na kisheria ili ili iweze kutamatisha kipindi cha mpito na kukaribisha demokrasia kamilifu, ukuaji wa uchumi, na utoaji huduma za umma. Haya yamejiri baada ya Baraza [...]

21/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hatua za kikanda zichukuliwe kuboresha usafi wa hewa maeneo ya Asia na Pasifiki: UNESCAP

Kusikiliza / Noeleen Heyzer

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi na Kijamii kwa ukanda wa Asia na pasifiki, ESCAP, Dr. Noeleen Heyzer, ametoa wito kwa nchi katika ukanda huo kutoa kipaumbele kwa usafi wa hewa na afya ya mwanadamu. Dr. Heyzer amesema afya ni kichochezi muhimu cha maendeleo, na kuongeza kuwa, katika juhudi za kujenga ukanda [...]

21/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya ukosefu wa chakula yazidi kushuhudiwa huko Palestina: WFP/UNRWA

Kusikiliza / gaza food

Wakuu wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa hii leo wameelezea hisia zao kutokana na kuendelea kushuhudiwa uhaba wa chakula katika ukingo wa magharibi wa mto Jordan na Gaza ambapo moja kati ya familia tatu za wapalestina zinakabiliwa ugumu wa kulisha familia zao. Jason Nyakundi na maelezo zaidi. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Ertharin Cousin Mkurugenzi [...]

21/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM na serikali ya Italia kuwasaidia kisikolojia waathirika wa vita vya Syria:

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, kwa msaada wa wizara ya mambo ya nje ya serikali ya Italia wamezindua mpango wa Euro milioni 1.5 ili kuwasaidia waathirika wa machafuko ya Syria.Msaada huo utakuwa ni wa kisaikolojia na utajumuisha walioko Syria na katika nchi jirani.Jumbe Omari Jumbe anafafanua zaidi (SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

21/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaonya juu ya hali mbaya ya usafi kwa wakimbizi wa ndani Syria

Kusikiliza / Watoto wa Syria wakiwa kambini

Zaidi ya watoto milioni 4 walioathirika na machafuko yaSyriawako katika hatari ya kupata maradhi ya kuambukiza kama kuhara kutokana na ukosefu wa majisafina vyoo limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Alice Kariuki na maelezo zaidi (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Shirika hilo linasema wakimbizi wengi wa ndani wa Syria na wale wanaoishi [...]

21/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031