Nyumbani » 20/06/2013 Entries posted on “Juni 20th, 2013”

Waasi washambulia zaidi baada ya serikali kuchukua hatamu za ulinzi Afganistan: UM

Kusikiliza / Jan Kubiš

Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa nchini humo Jan Kubiš amesema kwa sasa kuna dalili dhahiri shahiri kwa Jumuiya ya kimataifa kuendeleza usaidizi wake kwa Afghanistan hadi mwakani na zaidi kwa njia ambazo zitaimarisha uongozi wa nchi hiyo. (SAUTI YA Jan) “Kama ilivyotangazwa wiki hii, majeshi ya Afghanistani yameingia awamu ya mwisho ya kushika hatamu [...]

20/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Njaa katika dunia iliyojaaliwa ni kashifa:Papa Francis/FAO

Kusikiliza / Papa Francis alipokutana na washiriki mjini Vatican

Baba mtakatifu Francis amewataka washiriki kwenye mkutano wa 38 wa shirika la chakula na kilimo FAO kushirikiana kwa pamoja kupiga vita njaa, lakini pia kuchukua hatua zaidi ya tofauti zao katika sera ambazo hazijumuishia wanyonge na zinazochangia njaa na umasikini duniani. Akizungumza alipokutana na washiriki hao mjini Vatcan amesema ukweli ulio bayana kwamba kiwango cha [...]

20/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Makubaliano nchini Mali ni nuru kwa wananchi na ukanda mzima: UM

Kusikiliza / Kanali Moussa Sinko Coulibaly kutoka serikali ya Mali na Katibu Mkuu wa kikundi cha MNLA Bilal Ag Acherif

Huko Burkina  Faso wiki hii kulitiwa saini makubaliano ya amani kati ya serikali ya Mali na kundi la MNLA yanayoweka uwanja wa kuelekea kwenye uchaguzi wa rais na kuanzishwa kwa duru la mazungumzo ya amani baina ya serikali ya mpito na kundi la vugu vugu la kitaifa kwa ajili ya mali, MNLA. Je nini kilijiri? Ungana [...]

20/06/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lapongeza makubaliano ya Mali

Kusikiliza / Raia wa Mali

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limesema kuwa hatua ya kusainiwa makubaliano ya Ouagadougou ambayo yanaweka uwanja wa kuelekea kwenye uchaguzi wa rais na kuanzishwa kwa duru la mazungumzo ya amani baina ya serikali ya mpito na kundi la vugu vugu la kitaifa kwa ajili ya mali ,MNLA ni hatua inayopaswa kupongezwa. Baraza hilo [...]

20/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM, OIC na serikali ya Ufilipino washirikiana kuwasaidia watu nchini Ufilipino

Kusikiliza / Rashid Khalikov

  Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa ukiongozwa na serikali ya Ufilipino, muungano wa kislamu OIC , Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA na mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Ufilipino unakamilisha ziara yake hii leo. Ziara hiyo ilitoa fursa ya kutoa hamasisho kuhusu hali ya kibinadamu nchini Ufilipino [...]

20/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ukatili wa kingono dhidi ya wanawake ni tatizo la afya ya jamii duniani: WHO

Kusikiliza / Wanawake Burundi

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO na washirika wake imedhihirisha kuwa ukatili wa kingono au kimwili dhidi ya wanawake ni tatizo la afya ya jamii duniani ambalo huathiri zaidi ya theluthi moja ya wanawake duniani kote. George Njogopa anafafanua zaidi. (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA) Ikichambua mazingira ya wanawake kunyanyaswa, ripoti hiyo inasema kuwa [...]

20/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola Milioni 485 zahitajika kwa usaidizi wa kibinadamu huko Juba

Kusikiliza / Juba - Sudan Kusini

Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yaliyoko Sudan Kusini yanahitaji dola Milioni 485 hadi mwishoni mwa mwaka huu , ili kusaidia watu Milioni Tatu huko Juba kuweza kujenga upya maisha yao. Hiyo ni kwa kwa mujibu wa ripoti ya tathmini ya kati ya mwaka operesheni kubwa zaidi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa [...]

20/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Adha ya ukimbizi sio kwa mtu mmoja tuu bali ni kwa

Kusikiliza / Wakimbizi wa kisomali

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi na dunia nzima kwa ujumla wanaadhimisha siku ya wakimbizi duniani kwa kupongeza ushupavu na na ushujaaa wa watu zaidi ya milioni 40 duniani ambao wamelazimika kufungasha virago kutokana na vita au mauaji. Flora Nducha na taarifa kamili.  (RIPOTI YA FLORA NDUCHA) Kauli mbiu ya mwaka huu ni [...]

20/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shambulio la Moghadishu ni unyama usiokubalika:Ban

Kusikiliza / SG speaks to the press regarding the deadly attack on the world body’s compound in the Somali capital

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la Jumatano kwenye ofisi za Umoja wa mataifa mjini Moghadishu na kuliita ni unyama na ukatuili usioelezeka. Ameyasema hayo akiwa mjini Beijingwakati wa mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa Uchina Yang Jiechi. Ban ametoa pole kwa familia za wahanga na kuwatakia [...]

20/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta yasogezwa mbele

Kusikiliza / Uhuru Kenyatta

Hii leo Alhamisi huko The Hague, Uholanzi, Mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu, ICC imesogeza mbele hadi tarehe 12 Novemba mwaka huu siku ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. Kesi hiyo awali ilikuwa ianze kusikilizwa tarehe Tisa mwezi ujao.  Uamuzi huo unafuatia moja ya vitengo vya mahakama ya ICC [...]

20/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031