Nyumbani » 14/06/2013 Entries posted on “Juni 14th, 2013”

Wafanyakazi wa misaada wako njiani kuelekea Kachin Myanamr:OCHA

Kusikiliza / Watoto, Mynmar

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA limesema msafara wa malori 10 ya wafanyakazi wa misaada uko njiani kuelekea jimbo la Kachin nchini Myanmar. Msafara huo una jumla ya watu 5100 ukiwa umesheheni vifaa vya kuokoa maisha ya watu vikiwemo ambavyo sio chakula. OCHA inasema hivi sasa fursa ya kuwafikia wanaohitaji [...]

14/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kimataifa wa uhamiaji kuanza Juni 18:IOM

Kusikiliza / IOM kufanya mkutano kuhusu wahamiaji Geneva

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM limesema kuanzia Jumatatu Ijayo Juni 18 litafanya mkutano wa kimataifa mjini Geneva kuhusu wahamiaji. Kwa mujibu wa shirika hilo miongoni mwa ajenda kuu ni mchango wa wahamiaji hao katika mataifa waliyotoka. Imebainika kwamba wahamiaji hutuma nyumbani mambilioni ya dola kila mwaka. Katika mkutano huo mawairi mbalimbali wanaohusika na jamii [...]

14/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu duniani inatarajiwa kutimu biloni 9.6 ifikapo mwaka 2050

Kusikiliza / Idadi ya watu kuongezeka hadi bilioni 9.6 ifikapo mwaka 2050

Idadi ya sasa ya watu wote dunaiani ambayo ni bilioni 7.2 inatarajiwa kuongezeka kwa watu milioni moja zaidi kwa muda wa miaka 12 inayokuja na kufikia watu bilioni 9.6 ifikapo mwaka 2050 kwa mujibu wa ripoti mpya iliyozinduliwa hii leo huku ongezeko hilo likitarajiwa kushuhudiwa kwenye nchi zinazoendelea.Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa idadi ya watu [...]

14/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tanzania na harakati za kutokomeza ajira za watoto majumbani

Kusikiliza / Mfanyakazi wa nyumbani

Wiki hii dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ajira za watoto. Siku hiyo ilifanyika huku mkutano wa kimataifa wa 102 wa shirika la kazi duniani, ILO ukiendelea hukoGeneva, Uswisi. Maudhui ya mwaka huu ni kutokomeza ajira za watoto majumbani. ILO inasema kuwa watoto zaidi ya Milioni 10 na nusu wameajiriwa majumbani duniani kote na [...]

14/06/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mama Kikwete apokea tuzo kwa kuchochea mafanikio ya MDGs nchini Tanzania

Kusikiliza / Mama Salma Kikwete akipokea tuzo

  Mjini New York, Marekani, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete amepokea tuzo kutokana na mchango wake katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia, MDG yanayofikia ukomo mwaka 2015. Shuhuda wetu alikuwa Joseph Msami.(Ripoti ya Joseph)

14/06/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lapata Rais mpya

Kusikiliza / John William Ashe

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lapata Rais mpya Uchaguzi umefanyika hii leo wa kumpata Rais wa kikao cha Sitini na Nane cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa naye ni Dokta John William Ashe kutoka Antigua na Barbuda. Grece Kaneiya na ripoti kamili. (RIPOTI YA GRACE) Dkt. Ashe anashika wadhifa huo wakati huu ambapo [...]

14/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IPU yaendelea kufuatilia kesi dhidi ya wabunge Burundi

Kusikiliza / Jengo la IPU

Umoja wa mabunge duniani, IPU unaendelea kushinikiza kupatiwa suluhu kwa kesi za madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi zinazokabili wabunge 20 na mbunge mmoja wa zamani kama anavyoripoti George Njogopa.(Taarifa ya George Njogopa) Ujumbe huo ambao ni kamati ya Umoja wa Mabunge duniani unatazamiwa kuwasili nchini Burundi kuanzia june 17 na utasalia [...]

14/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Misaada ya UNICEF haifikii familia za vijijini huko Damascus

Kusikiliza / Familia iliyopoteza makazi

Takribani raia Milioni Moja nukta Mbili wa Syriawanaoishi maeneo ya vijijini mashariki mwa mji mkuu waSyria,Damascusbado wana mahitaji makubwa ya kibinadamu, na hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF. Yaelezwa ya kwamba misafara ya Umoja wa Mataifa ikielekea maeneo hayo ikiwa na misaada kwa familia Elfu Tano imekwama [...]

14/06/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM waitaka Belarus kuheshimu haki za binadamu.

Kusikiliza / Miklos Haraszti

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa juu ya hali ya haki za binadamu nchini Belarus Miklos Haraszti, ameitaka nchi hiyo kutumia vyombo vyake kuhakikisha kwamba suala la haki za binadamu linaboreshwa.  Bwana Haraszti amesema kuwa mamlaka za dola pamoja na taasisi zake zimeendelea kubana haki za binadamu na wakati mwingine mamlaka hizo zinaweka ngumu wakati [...]

14/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM Imekamilisha tathimini ya maeneo yanayohifadhi wakimbizi Lebanon:

Kusikiliza / Nembo ya IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema limekamilisha tathimini ya haraka ya maeneo matano Kusini mwa Lebanon ambayo yanahifadhi wakimbizi toka Syria.Matokeo ya tathmini hiyo kwa mujibu wa IOM yanaashiria kwamba jamii za wakimbizi maeneo ya Saida na Sarafand yanahitaji msaada wa haraka ikiwemo malazi na vifaa visivyo chakula, huduma za afya, elimu ya usafi [...]

14/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yakamilisha kuwahamisha wakimbizi wa Darfur kutoka kwenye mpaka na Chad:

Kusikiliza / UNHCR yawahamisha wakimbizi wa Darfur kuelekea kambi mpya

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limemaliza zoezi la kuwahamisha wakimbizi wa Darfur kutoka katika eneo la machafuko la mpakani mwa Chad la Tissi.Wakimbizi hao wamepelekwa katika kambi mpya ya Ab Gadam ambayo sasa inahifadhi wakimbizi 10,247. Mbali ya sababu za kiusalama zilizochangia pakubwa kuhamishwa kwa wakimbizi hao UNHCR inasema eneo [...]

14/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msaada wa UNHCR wafika Al Raqqa nchini Syria

Kusikiliza / Familia ikichukua msaada wa hema huko Al Qusayr

Huduma za Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR zimefika Al Raqqa  eneo lililo kaskazini mwaSyriaambalo imekuwa vigumu kulifikia kwa muda wa miezi mitatu iliyopita na ambapo hali ya kibinadamu inaripotiwa kuwa mbaya. Alice Kariuki anaripoti (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Msaada huo utawasaidia karibu watu 5000 waliohama makwao eneohilo. Pia makundi ya UNHCR [...]

14/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031