Nyumbani » 12/06/2013 Entries posted on “Juni 12th, 2013”

Luteni Jenerali Babacar Gaye kuongoza BINUCA

Kusikiliza / Babacar Gaye, Mwakilishi maalum mpya wa Katibu Mkuu wa UM huko Jamhuri ya Afrika ya Kati

Baada ya kuongoza kikosi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC, MONUSCO, Luteni Jenerali Babacar Gaye kutokaSenegalsasa ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuwa Mwakilishi  wake huko jamhuri ya Afrika ya Kati.  Taarifa iliyotolewa New York, imesema Luteni Jenerali Gaye ambaye sasa ni msaidizi wa [...]

12/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu kwa Lugha ya Kiswahili yazinduliwa

Kusikiliza / Uzinduzi wa muhtasari wa Kiswahili wa ripoti ya UNDP

  Toleo la muhtasari wa ripoti ya maendeleo ya binadamu duniani imezinduliwa leo katika Chuo kikuu cha Pwani nchini Kenya. Hii ni mara ya kwanza ripoti hii imechapishwa kwa lugha ya Kiswahili. Lugha ya kiswahili inazungumzwa na zaidi ya watu milioni mia moja na hamsini, wengi wakiwa  katika eneo la Africa Mashariki, Afrika ya Kati [...]

12/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Côte d'Ivoire mwelekeo ni mzuri lakini bado kuna mparaganyiko: Mtaalamu UM

Kusikiliza / Doudou Diène

Mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa Doudou Diène ameeleza wasiwasi wake juu ya mparaganyiko wa kisiasa nchini Côte d'Ivoire akitaka kuwepo kwa usawa wa haki ndani ya nchi hiyo ambayo ameielezea sasa ina mgawanyiko baada ya msukosuko.  Akiwasilisha ripoti yake kwenye kikao cha 23 cha Baraza la haki za binadamu mjini Geneva, Uswisi, Diène amesema [...]

12/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Malawi yaahidi kuchochea utokomezaji ajira kwa watoto majumbani

Kusikiliza / Rais Joyce Banda wa Malawi

Wakati dunia hii leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ajira kwa watoto, Rais Joyce Banda wa Malawi amezungumza katika mkutano wa 102 wa kimataifa wa shirika la kazi duniani, ILO na kusema nchi yake itachochea harakati za kupiga vita vitendo hivyo dhalimu kwa watoto vinavyowanyima haki zao za msingi ikiwemo kwenda shule. Assumpta Massoi [...]

12/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya Mali na makundi ya waasi walikiuka haki za binadamu: UM

Kusikiliza / Flavia Pansieri

Umoja wa Mataifa umeorodhesha visa kadha vinavyokisiwa kukiuka haki za binadamu vilivyotekelezwa na wanajeshi nchiniMaliwakati wa oparesheni zao za kuwatimua waasi  waliokuwa wamechukua udhibiti maneo ya kaskazini mwa nchi. Jason Nyakundi anaripoti.  (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Uchunguzi ulioendeshwea na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa umebainisha kuwa vikosi vya serikali viliendesha mauaji [...]

12/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nchi 38 zatimiza lengo la kuangamzia njaa kabla ya ukomo uliowekwa:FAO

Kusikiliza / mahindi barani Afrika

Jumla ya nchi 38 zimetimiza malengo ya kimataifa ya kupambana na njaa kabla ya muda uliowekwa 2015 kwa mujibu wa Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO. Mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano da Silva anasema kuwa mataifa hayo ni ishara kuwa kujitolea kisiasa , uongozi mwema na ushirikinao  inakuwa ni rahisi [...]

12/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mipango ya maendeleo izingatie utamaduni wa watu: UM

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki Moon na Rais wa Baraza Kuu la UM Vuk Jeremic

Hapa mjini New York, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili uhusiano kati ya utamaduni na maendeleo. Joshua Mmali amekuwa akiufuatilia mjadala huo. TAARIFA YA JOSHUA MMALI Katika hotuba yake ya kufungua kikao cha leo cha Baraza Kuu, rais wa BarazahiloVuk Jeremic, ametoa wito kwa nchi wanachama ziifanye ajenda ya maendeleo baada ya mwaka [...]

12/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa mataifa una wasiwasi na ukiukwaji wa haki za binadamu Sudan Kusini

Kusikiliza / UM kulinda haki za raia Sudan Kusini

Hali ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini bado si nzuri wakati huu ambapo serikali inahaha kulinda raia dhidi ya vitendo vya ghasia,  na hiyo ni kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kama anavyoelezea George Njogopa.(TAARIFA YA GEORGE) Akizungumzia hali jumla ya mambo katika eneo hilo, Naibu Mkuu wa [...]

12/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Twahitaji wachangiaji damu hiari: WHO

Kusikiliza / Siku ya kutoa damu kwa hiari Juni 14

Mahitaji ya damu yanaongezeka kila mwaka na mamilioni ya wanaohitaji huduma hiyo ili kuokoa maisha yao hawapati kwa wakati, na hiyo ni taarifa ya shirika la afya duniani, WHO katika kuelekea siku ya kimataifa ya uchangiaji damu kwa hiari tarehe 14 mwezi huu. WHO inasema mwaka 2011 walikusanya takribani michango hiari ya damu Milioni 83 duniani [...]

12/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930