Nyumbani » 11/06/2013 Entries posted on “Juni 11th, 2013”

Ajira za watoto majumbani zikomeshwe: ILO

Kusikiliza / Ajira kwa watoto haifai. ILO

Kufua nguo, kuteka maji, kulea watoto wenzao na hata kulea wazee, ni majukumu ambayo Shirika la kazi duniani, ILO limetaja katika ripoti yake kuwa yanakabili watoto walioajiriwa majumbani kinyume cha sheria na kutumikishwa kama watumwa.Ripoti hiyo ambayo inazinduliwa leo siku ya kimataifa ya kutokomeza ajira kwa watoto inaitwa Kutokomeza ajira za watoto majumbani na inasema [...]

11/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ICTR kuendelea kuwasaka watuhumiwa wa mauaji

Kusikiliza / Ofisi ya ICTR

Licha ya Mahakama ya kimataifa ya Rwanda ICTR iliyokuwa na makao yake makuu mjini Arusha, Tanzania kumaliza muda wake watuhumiwa tisa wanaendelea kusakwa kwa garama yoyote ili kufikishwa mahakani. Akongea na waandishi wa habari mjini New York , mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo Hasani Jallow amesema ICTR ambayo imewafungulia mashtaka jumla ya watuhumiwa 93 imekamilisha [...]

11/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tanzania yaangazia ajira kwa vijana wakati mkutano wa ILO ukiendelea

Kusikiliza / Eric Shitindi

Wakati mkutano wa 102 wa Shirika la kazi duniani ILO ukiendelea mjini Geneva mwakilishi wa serikali ya Tanzani katika mkutano huo Katibu wa wizara ya Kazi wa Tanzania Eric Shitindi anasema licha ya changamoto kadhaa za kazi zinazoikumba nchi hiyo iliyoko Afrika Mashariki , mkutano huo utatumiwa kuisaida nchi hiyo kupiga hatua katika kusaidia makundi [...]

11/06/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ukanda wa Sahel wakabiliwa na njaa, magonjwa na vita -Piper

Kusikiliza / Wakazi wa Ukanda wa Sahel barani Afrika

Mratibu wa misada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Sahel Robert Piper amesema ukanda huo unakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula, hali mbaya ya usalama na magonjwa na kwamba kiasi cha dola bilioni moja nukta saba kinahitajika kusaidia watu wa eneo hilo. Akiongea na waandishi wa habari mjini New York [...]

11/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na machafuko Iraq

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema amekuwa akifuatilia kwa masikitiko matukio ya kisiasa na kiusalama yanayoibuka nchini Iraq, yakiwemo kuongezeka kwa hali tete kisiasa na machafuko yalosababisha idadi kubwa ya vifo katika kipindi cha miezi miwili ilopita. Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban ametuma risala ya pole kwa waathiriwa [...]

11/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaangazia maisha ya watoto walemavu Mali.

Kusikiliza / UNICEF yawasaidia watoto walemavu Mali

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limejikita katika kuwasaidia watoto walemavu nchini Mali kwa kuanzisha shule maalum inayofundisha watoto hao katika eneo la Bamako. Ungana na Joseph Msami katika makala hii inayomuangazia mmoja wa watoto mwenye miaka 11 amabaye ni mlemavu wa kusikia anayesoma katika shule hiyo.

11/06/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lajadili Yemen

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali nchiniYemen, wakati Ofisi ya kuratibu misaada ya kibindamu, OCHA ikisema idadi ya wakimbizi wa ndani nchini humo imepungua, kwa kiasi kikubwa. Joshua Mmali na taarifa zaidiTAARIFA YA JOSHUA Yemenndiyo nchi pekee iloweza kujiibua kutoka kwenye machafuko na makubaliano yalotokana na mazungumzo ya amani, pamoja na [...]

11/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Indonesia bado yakabiliwa na changamoto ya makazi bora

Kusikiliza / Moja ya vitongoji kwenye mji mkuu wa Indonesia, Jakarta

Indonesia imetajwa kuwa inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha kwamba inaendeleza na kulinda haki za kupata makazi bora miongoni mwa wananchi wake hali ambayo imesababishwa na ukuaji wa kasi wa miji na kukosekana kwa mipango endelevu. Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa Raquel Rolnik amesema kuwa kutokana na hali hiyoIndonesiainakabiliwa na majanga ya kimazingira yatokanayo [...]

11/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania yamulika ajira ya vijana katika mkutano wa ILO

Kusikiliza / Tanzania yaangazia ajira kwa vijana mkutanoni,ILO

Wakati mkutano mkuu wa 102 wa shirika la kazi duniani ILO ukiendelea mjini Geneva, Tanzania inatarajia kutumia mkutano huo kuimarisha ajira za vijana. Katika mahojiano maalum na idhaa hii Mwakilishi wa serikali ya Tanzania Eric Shitindi amesema ajira kwa vijana ndio changamoto kuu na kwamba kupitia mkutano huo wanatarajia kujifunza na kupata mbinu mpya za [...]

11/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Noeleen Heyzer sasa kuwa mshauri maalumu wa UM Timor-leste:

Kusikiliza / Noeleen Heyzer

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza kuwa amemteua Bi. Noeleen Heyzer raia wa Singapore ambaye kwa sasa ni katibu mkuu wa tume ya uchumi na jamii kwa mataifa ya Asia na Pacific kuwa mshauri wake maalumu kwa ajili ya Timor-Leste. Pamoja na majukumu hayo mapya Bi. Hayzer ataendelea kuwa katibu mkuu wa [...]

11/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mitaala ya shule ijenge utangamano baina ya makundi badala ya ubaguzi: Ruteere

Kusikiliza / Ubaguzi wa aina yeyote haufai,Ruteere

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ubaguzi wa rangi, chuki za watu wa kigeni na aina zingine za ubaguzi, Mutuma Ruteere amezungumzia nafasi ya elimu katika kutokomeza vitendo vya ubaguzi na chuki kwenye maeneo mbali mbali duniani. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.(Taarifa ya Assumpta) Ni kwenye kikao cha baraza la haki [...]

11/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNFPA yaomba dola milioni 40 kwa ukunga na dhuluma za kijinsia Syria

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria

Shirika la Idadi ya Watu katika Umoja wa Mataifa, UNFPA, linajitahidi kuokoa maisha ya akina mama waja wazito kwa kutoa huduma zinazozuia vifo vya akina mama katika uzazi, pamoja na dhuluma za kijinsia kwa wakimbizi wa ndani na nje ya Syria. Joshua mmali na maelezo zaidi(RIPOTI YA JOSHUA MMALI) UNFPA imesema, miongoni mwa idadi ya [...]

11/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Asilimia 90 ya wakimbizi wa ndani warejea makwao Yemen: OCHA

Kusikiliza / Familia zilizokuwa zinaishi kwenye kambi huko Abyan

Zaidi ya asilimia 90 ya wakimbizi wa ndani wamerejea kwenye jimbo la Abyan kusini mwaYemen baada ya kupungua kwa ghasia , kurejea kwa huduma na pia kufunguliwa kwa masoko. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA ni kwamba idadi ya wakimbizi wa ndani  kusini mwaYemenimepungua kutoka watu 68,533 mwezi [...]

11/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Msako wa Boko Haram wasababisha raia Elfu Sita kukimbia makazi yao Nigeria

Kusikiliza / Askari nchini Nigeria

Nchini Nigeria zaidi ya watu Elfu Sita wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee wamekimbia makaziyaokaskazini mwa nchi hiyo na kuelekeaNigerkwa hofu ya usalama wao. Kulikoni, tujiunge na George Njogopa kwa maelezo zaidi. (TAARIFA YA GEORGE) Watu hao wameliambia shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR kuwa wamelazimika kukimbia kwa hofu ya kukamatwa [...]

11/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yahofia usalama wa raia waliokimbia mapigano Jonglei:

Kusikiliza / Mabaki ya nyumba baada ya mapigano huko Jonglei, Sudan Kusini

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema lina shaka kubwa juu usalama wa raia waliokimbia makwao hukoJonglei,SudanKusini kutokana na mapigano yanayoendelea tangu mwezi Machi kati ya majeshi  ya serikali na vikundi vyenye silaha. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (RIPOTI YA GRACE KANEIYA) Maelfu ya raia wanaripotiwa kukimbia na kuwa wakimbizi wa ndani [...]

11/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 1.5 wanashida ya chakula Haiti:WFP

Kusikiliza / wananchi wa Haiti wakiwa kwenye foleni wakisubiri mgao wa chakula na dawa

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linatiwa hofu na hali ya watu milioni 1.5 wanaochukuliwa kuwa na shida ya chakulaHaiti. Shirika hilo linasema kunatabiriwa kuwa na hali mbaya ya hewa hasa katika msimu huu wa vimbunga kuanzia Juni hadi Novemba na WFP inajiandaa kusambaza msaada wa chakula na kutoa msaada wa kibinadamu ikishirikiana [...]

11/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031