Nyumbani » 10/06/2013 Entries posted on “Juni 10th, 2013”

Nasikitishwa na jamii zinazonyanyapaa wagonjwa wa Ukimwi: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza katika kikao cha Baraza Kuu cha kutathmini utekelezaji wa maazimio ya hatua thabiti dhidi ya ukimwi na utashi wa kisiasa dhidi ya ugonjwa huo ya mwaka 2011 na kusema kuwa miaka miwili baada ya tamko hilo bado kuna nchi ambazo zinaendeleza sera za unyanyapaa na  ubaguzi [...]

10/06/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UM wahofia watoto 53 DRC kusajiliwa tena na waasi wa M23

Kusikiliza / Kuna wasiwsi kufuatia ripoti ya kusajiliwa kwa watoto 53,na kundi la M23

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSO pamoja na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu watoto katika vita vya silaha, Leila Zerrougui, wameelezea wasiwasi kufuatia ripoti zinazoonyesha kuwa yapata watoto 53 wapo katika hatari ya kusajiliwa tena na kundi la waasi wa M23, kwenye eneo la Nyiragongo, [...]

10/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kay akutana na wanaharakati Somalia

Kusikiliza / Somalia, Kay alikokutanan na wanaharakati

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay amewasili nchini humo tayari kuanza kazi ambapo miongoni mwa kazi za awali alizofanya ni kukutana na wawakilishi wa makundi ya wanaharakati. Ungana na Joseph Msami katika taarifa hii inayofuatilia ziara hii ya Kay ambaye aliteuliwa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Umoja wa [...]

10/06/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Kobler kuwa mwakilishi wa UM wa MONUSCO

Kusikiliza / Martin Kobler

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jumatatu ametangaza kwamba amemteua Martin Kobler raia wa Ujerumani kuwa mwakilishi wake maalumu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO). Mwakilishi huyo mpya atachukua nafasi ya Roger Meece kutoka Marekani ambaye atakamilisha muda wake Julai mwaka huu. Katibu Mkuu amesema anashukuru kwa kazi [...]

10/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa katibu mkuu wa UM ataka kusitishwa mapigano mjini Kismayo

Kusikiliza / Nicholas Kay

  Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay ametaka kusitishwa kwa mapigano mjini Kismayo kufutaia kuripotiwa tena kwa mapigano . Kay anazitaka pande zote husika kutatua tofauti zao kwa njia ya amani. Anasema kuwa hali ya sasa nchini Somalia inastahili kuwa ambayo matatizo yanatatuliwa kwa njia ya amani. Anasema [...]

10/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mikakati thabiti yahitajika kupunguza ukosefu wa usawa kama chanzo kikuu cha umaskini

Kusikiliza / poverty unequality

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wamepongeza utambuzi wa umuhimu wa usawa kama msingi wa ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015, kama ilivyobainishwa kwenye ripoti muhimu ya Umoja wa Mataifa. Hata hivyo wametaka viongozi wa dunia kuridhia hatua madhubuti kutokomeza ukosefu wa usawa. Grace Kaneiya anafafanua zaidi.  RIPOTI [...]

10/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali zawajibika kuchunguza na kuzuia ukatili dhidi ya wanawake

Kusikiliza / Rashida Manjoo

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake amesema serikali zinapaswa kuwajibika siyo tu kwa kuchunguza ukatili dhidi ya wanawake bali pia kwa kuwajibishwa kwa kushindwa kuzuia kutokea kwa vitendo hiyo. Rashinda Manjoo akizungumza mjini Geneva, Uswisi amesema kuwajibishwa huko kunatokana na serikali kushindwa kudhibiti mifumo iliyopo inayofanywa zishindwe kuzuia ukatili dhidi [...]

10/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNEP yakaribisha ushirikiano wa Marekani na Uchina kudhibiti mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / Marais wa Marekani na Uchina wakutana kujadili ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi

Mkuu wa Shirika la Mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, UNEP, Achim Steiner, amekaribisha uamuzi wa kuwepo ushirikiano kati ya Uchina na Marekani katika kukomesha matumizi ya aina ya fulani za kemikali ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi .Bwana Steiner amesema tangazo la ushirikiano huo, ambalo limefanywa na Rais Barack Obama wa Marekani na [...]

10/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kongamano London latoa matumaini ya vita dhidi ya kudumaa na lishe duni kwa watoto:

Kusikiliza / child weigh

Kongamano lililofanyika London mwishoni mwa wiki kuhusu lishe kwa ukuaji limetoa fursa mpya ya kupunguza zaidi athari za kudumaa na mifumo mingine ya lishe duni kwa mamilioni ya watoto. Hayo yamesema na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, likiongeza kuwa kwa watoto wanaokabiliwa na tishio lisilostahili la kudumaa, maradhi ambayo sio tuu [...]

10/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wapalestina elfu Tano wanaoshikiliwa Israel wanaishi maisha dhalili

Kusikiliza / palestine-demolition

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa ametaka kuundwa kwa tume ya kuchunguza hali ya takribani wapalestina Elfu Tano wanaoshikiliwa au kufungwa nchini Israel kwa madai kuwa maisha yao ni dhalili na ya taabu. Taarifa ya George Njogopa inafafanua zaidi. (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA) Richard Falk ambaye ni mtaalamu huru wa masuala ya haki za binadamu [...]

10/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano Dakar watathmini maendeleo ya haki ya chakula Afrika Magharibi

Kusikiliza / food index

Zaidi ya washiriki 40 wakiwemo wabunge, maafisa wa serikali na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiraia wanakutana Dakar, Senegal kuangalia mbinu bora za kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha kutosha kama haki ya binadamu. Jason Nyakundi na ripoti zaidi. (TAARIFA YA JASON) Mkutano huo ulioitishwa na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa [...]

10/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wataka amani Benghazi

Kusikiliza / Ramana ya Libya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya UNSMIL umeelezea hali ya wasiwasi wake kutokana na kuongezeka kwa mapigano yanayoukumba mji wa Benghazi na umetaka kurejeshwa kwa hali ya utulivu. Watu kadhaa wameripotiwa kufariki duniani na wengine kujeruhiwa vibaya ikiwa ni matokeo ya machafuko yanayolikumba eneo hilo. Katika taarifa yake, UNSMIL umetaka pande zinazohasimiana [...]

10/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yataja maadui wa afya ya umma duniani

Kusikiliza / Margaret han

Mkutano wa Nane wa dunia kuhusu uboreshaji wa afya umeanza Jumatatu huko Finland ukimulika zaidi mwelekeo wa afya ya jamii ambao ni msingi wa jamii kuwa na afya bora. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.  (TAARIFA YA ASSUMPTA) Mkutano huo ulioandaliwa kwa pamoja na WHO na Finland unaangalia kile ambacho serikali zinapaswa kufanya ili kuboresha [...]

10/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031