Nyumbani » 05/06/2013 Entries posted on “Juni 5th, 2013”

Ban ampongeza Rice, aelezea uthabiti wake

Kusikiliza / Balozi Susan Rice

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amempongeza Bi Susan Rice kufuatia kuteuliwa kwake kuwa mshauri wa usalama wa taifa wa serikali ya Marekani . Bwana Ban amempongeza Rice kwa utendaji wake mzuri wakati akitumika katika nafasi ya mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2009 akimtaja kama sauti [...]

05/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usindikaji vyakula umekuwa bora baada ya kupata mafunzo: Wajasiriamali wanawake Tanzania

Kusikiliza / Kiwandani cha chakula

Usaidizi huo uliohusisha pia mfuko wa mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) na serikali ya Tanzania umefanyika kupitia mfuko wa umoja wa udhamini wa wanawake wasindikaji wa vyakula Tanzania, TWFPT. Katika mahojiano haya mwenyekiti wa mfuko huo Emmy Kiula anamweleza Stephanie Raison wa UN-Women Tanzania kile wanachofanya na manufaa waliyopata bila kusahau changamoto.

05/06/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yaungana na dunia kuadhimisha siku ya mazingira.

Kusikiliza / UNEP_logo-298x300

Nchi mbalimbali duniani leo zimeadhimisha siku ya mazingira duniani zikichagizwa na kauli mbiu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP “kufikiri, kula, kuhifadhi mazingira na kupunguza uharibifu wa chakula katika jamii” Nchini Tanzania siku hii imeadhimishwa kwa kwa hamasa ya kuhifadhi mazingira kulingana na kauli mbiu hiyo kama anavyoeleza naibu katibu mkuu wa [...]

05/06/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ajira bado changamoto duniani -ILO

Kusikiliza / Guy Ryder

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kazi duniani ILO Guy Ryder amesema kumekuwa na mabadiliko makubwa na ya kasi katika ajira duniani kufuatia kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa kazi miongoni mwa watu,teknolojia , kukosekana kwa usawa, umaskini na ukuaji mdogo wa uchumi. Akiongea wakati wa ufunguzi wa kongamano la kimataifa la 102 la kimataifa kuhusu ajira [...]

05/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa mpangilio wa kukabiliana na uzito wa juu wa mwili miongoni mwa watoto

Kusikiliza / obesity

Nchi nyingi zenye kipato cha chini na cha wastani zimetupilia mbali masuala ya uzito wa mwili kupita kiasi na athari zake kwa afya wakati kukiwa na sera za kukabiliana na ukosefu wa lishe wakati pia ambapo kuna ukosefu wa sera za kuzuia magonjwa yanayosababishwa na uzito wa juu wa mwili kwa mujibu wa taarifa mpya [...]

05/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano kuhusu Syria sasa kufanyika penginepo Julai na si mwezi huu: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Mkutano wa kimataifa kuhusu Syria uliokuwa ufanyike mwezi huu huko Geneva, sasa utafanyika penginepo mwezi ujao kwa sababu maandalizi hayajakamilika. Taarifa hizo zimetolewa na mjumbe maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu, Lakhdar Brahimi alipokutana na waandishi wa habari baada ya mazungumzo ya utatu ya maandalizi baina ya Urusi, Marekani na [...]

05/06/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili hali nchini Sudan:

Kusikiliza / Fatou Bensouda, Mwendesah mashtaka mkuu wa ICC

 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limekutana kujadili hali katika eneo la Darfur nchini Sudan, pamoja na kupitisha kwa kauli moja, azimio kuhusu kutosambaza silaha. Joshua Mmali amekuwa akifuatilia matukio hayo na hapa ni taarifa yake. (Ripoti ya Joshua Mmali)

05/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waziri wa kazi wa Jordan achaguliwa kuongoza mkutano wa kimataifa wa ILO

Kusikiliza / Mkutano wa kimataifa wa ILO

Waziri wa kazi na usafiri wa Jordan Dr Nidal Katamine amechaguliwa kuwa Rais wa mkutano wa 102 wa kimataifa wa shirika la kazi duniani ILO ulioanza leo na kuhitimishwa Juni 20. George Njogopa na taarifa kamili.(TAARIFA YA GEORGE) Katika hotuba yake ya ufunguzi wa kongamano hilo la kimataifa, Dk Katamine amesema kuwa miongoni vya vipaumbele [...]

05/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia Elfu Nne wa Eritrea hukimbia nchi yao kila mwezi

Kusikiliza / Hadi watu elfu nne wakiwemo watoto hukimbia ukosefu uhuru, Eritrea

Hali ya usimamizi wa haki za binadamu nchini Eritrea inazidi kuporomoka kila uchwao na hivyo ndivyo baraza la haki za binadamu limeelezwa huko Geneva, Uswisi na mtaalamu huru wa haki za binadamu na kusababisha maelfu ya raia kukimbia nchi hiyo. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi.  (RIPOTI YA ALICE KARIUKI) Mtaalamu huru wa Umoja wa [...]

05/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wajasiriamali wanawake Tanzania waelezea wanavyonufaika na mpango wa UM

Kusikiliza / Wajasiriamali wanawake wakichambua korosho

Mkutano wa kimataifa kuhusu uwiano sawa wa kijinsia katika maendeleo unaanza nchini Tanzania kesho chini ya mhimili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN-WOMEN na mfuko wa maendeleo ya mitaji wa Umoja wa Mataifa, UNCDF.Mkutano huo unafanyika wakati taasisi hizo mbili kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania zimetoa mafunzo ya kuboresha [...]

05/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais wa Ufaransa kutunukiwa tuzo inayotambuliwa na UNESCO

Kusikiliza / French president

Rais wa Ufaransa Francois Hollande leo anatazamiwa kutunukiwa tuzo ya amani ya Félix Houphouët-Boigny wakati wa sherehe maalumu zitazofanyika kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO.  Tuzo hiyo iliasisiwa mwaka 1989 hutolewa mahasusi kwa watu ama taasisi zilizotoa mchango mkubwa wa upatikanaji wa amani duniani. Miongoni [...]

05/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Fikiri, Kula, hifadhi Mazingira; Punguza Uharibifu wa chakula

Kusikiliza / UNembo ya siku ya mazingira:NEP

  Katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani leo Juni Tano shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP limeitaka "kufikiri, kula, kuhifadhi mazingira na kupunguza uharibifu wa chakula katika jamii" ikiwa ndio kauli mbiu ya mwaka huu. Flora Nducha na ripoti kamili (RIPOTI YA FLORA NDUCHA)  Kauli hiyo ni ya kuchagiza kila mtu kupunguza upotevu [...]

05/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031