Nyumbani » 03/06/2013 Entries posted on “Juni 3rd, 2013”

Tusaini mkataba wa biashara ya silaha kwa maslahi ya wote: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM, Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitaka nchi wanachama wa umoja huo kujitokeza kwa wingi kutia saini mkataba wa kimataifa kuhusu biashara ya silaha, ATT, ulioanza kutiwa saini leo baada ya kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Aprili mwaka huu. Akizungumza mjini New York, Marekani siku ya Jumatatu baada ya [...]

03/06/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Virusi vya polio vyabainika Israel:WHO

Kusikiliza / WHO LOGO

  Virusi vya polio aina ya 1(WPV1) vimebainika katika sampuli za maji taka yaliyokusanywa April9 mwaka huu Kusini mwa Israel. Virusi hivyo vimebainika kwenye maji taka pekee hakuna tukio lolote la kupooza lililoripotiwa. Uchunguzi unaendelea ili kujua chanzo cha virusi hivyo kwani uchunguzi wa awali umebaini kwamba virusi hivyo havina uhusiano na vile vinavyoathiri Pembe [...]

03/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waziri mkuu wa china azungumzia njia za kuboresha uchumi duniani

Kusikiliza / Waziri Mkuu wa Uchina Li Keqiang

Waziri mkuu nchini China Li Keqiang anasema kuwa sekta za kutoa huduma kote duniani zinaweza zikatoa fursa muhimu kwa ukuaji wa uchumi fursa inayohitajika na nchi zinazoendelea. Akihutubi mkutano wa kimataifa kuhusu huduma bwana Li amesema kuwa mabadiliko yanahitajika kufanywa katika sekta ya utoaji huduma ili kuweza kubuni nafasi zaidi za ajira. Ameuambia mkutano huo [...]

03/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Balozi Mahiga azungumzia Afrika na utatuzi wa migogoro

Kusikiliza / Augustine Mahiga

Hatimaye muda wa huduma ya Ofisi ya kisiasa ya Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, UNPOS, umemalizika na kuanzia Jumatatu, Juni 3, ujumbe mpya wa Umoja wa Mataifa wa kuisaidia Somalia, UNSOM, utaanza majukumu yake.Balozi Augustine Mahiga ambaye aliongoza UNPOS amesema ulikuwa ni uzoefu wa kipekee na anashukuru kuwa ameweze kusongesha mchakato wa kisiasa hadi hivi [...]

03/06/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa Biashara ya Silaha waanza kutekelezwa

Kusikiliza / Mkataba wa biashara ya silaha wafanyika, Baraza Kuu la UM

Mkataba wa biashara ya silaha, ambao ni wa kwanza wa aina yake kujadiliwa na kuamuliwa katika Umoja wa Mataifa, ulipitishwa mnamo tarehe 2 Aprili mwaka huu. Leo Juni 3, nchi nyingi wanachama zimejitokeza kuutia saini, na hivyo kuanza rasmi kutekelezwa kwa mkataba huo. Akiongea wakati wa hafla hiyo, Bi Angela Kane, ambaye ni Mwakilishi Mkuu [...]

03/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Profesa kutoka Afrika Kusini kuongoza jopo la wanasayansi dhidi ya Ukimwi

Kusikiliza / Salim S Abdool Karim

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa umoja wa Mataifa linaloratibu masuala ya Ukimwi, UNAIDS Michel Sidibé ametangaza uteuzi wa Profesa Salim S Abdool Karim kutoka Afrika Kusini kuongoza jopo la wanasayansi kuhusu Ukimwi. Ripoti ya George Njogopa inafafanua zaidi. (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

03/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe mpya wa UM awasili nchini Somalia

Kusikiliza / Nicholas Kay

Mjumbe mpya wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Nicholas Kay amewasili nchini Somalia hii leo kuchukua wadhifa wake kama mkuu wa ujumbe wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM.Alipowasili mjumbe huyo wa katibu mkuu amesema amefurahishwa kuwa mjini Mogadishu  na kwa kupewa fursa hiyo  kuisaidia serikali na watu wa Somalia katika kuleta [...]

03/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ILO:Kutokuwepo na uwiano katika upatikanaji ajira ni changamoto

Kusikiliza / Kuna tatizo la ukosefu wa ajira kote ulimwenguni, ILO

Shirika la kazi duniani, ILO limetoa ripoti yake inayoeleza kuwa  watu zaidi ya Milioni Nane wataingia katika kundi la wasio na ajira katika kipindi cha miaka miwili ijayo na kufanya idadi ya watu wasio na ajira duniani kufikia Milioni 208 . Hii ni kutokana na harakati za kujikwamua kutoka mdororo wa kiuchumi duniani kuendelea kusuasua. [...]

03/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMA imelaani vikali shambulio Mashariki mwa Afghanistan:

Kusikiliza / Ján Kubiš

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Afghanistan UNAMA imelaani vikali mashambulio mawili ya mabomu yaliyofanyika leo Jumatatu Mashariki mwa nchi hiyo na kukatili maisha ya watu 19 wakiwemo watoto zaidi ya 10, yakidhihirisha kwa mara nyingine kuwa wapinzani wa serikali wanalenga maeneo ya raia.Akizungumzia mashambulizi hayo mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na [...]

03/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa IAEA yawasilisha ripoti kwa bodi ya magavana:

Kusikiliza / Ripoti kuhusu masula ya nyuklia yawasilishwa

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic Yukiya Amano Jumatatu amewasilisha taarifa kwenye bodi ya magavana wa shirika hilo.Katika taarifa hiyo bwana Amano amewaambia nchi wanachama wa IAEA kuhusu masuala ya ukaguzi wa nyuklia ikiwemo nchini Iran na Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK. Ametangaza kuwa kongamano la kisayansi la [...]

03/06/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Utegemezi wa misaada kutatua migogoro unakwamisha jitihada za amani Afrika: Mahiga

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga

 Baada ya kuhitimisha jukumu lake la miaka mitatu akiongoza ofisi ya kisiasa ya Umoja wa Mataifa nchiniSomalia, UNPOS, Balozi Augustine Mahiga amezungumzia kile ambacho nchi za Afrika zinapaswa kufanya katika utatuzi wa migogoro inayokabili bara hilo.   Balozi Mahiga amesema hayo katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa wakati akizungumzia uzoefu wake na kile [...]

03/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yaeleza wasiwasi wa uharibifu wa maeneo ya kihistoria Syria

Kusikiliza / Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO

Wakati ripoti za kuharibiwa kwa maeneo kadhaa ya kihistoria na kidini nchini Syria zikiendelea kutolewa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limetaka maeneo hayo kulindwa dhidi ya mashambulizi yanayoendelea. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova kwa kauli yake amesema ana wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya maeneo hayo ya kihistoria [...]

03/06/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031