Nyumbani » 02/06/2013 Entries posted on “Juni 2nd, 2013”

Muda wa UNPOS wamalizika, UNSOM kuanza majukumu Somalia Juni 3

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud

Muda wa huduma ya Ofisi ya kisiasa ya Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, UNPOS, umemalizika leo, Juni 2. Kuanzia Jumatatu, Juni 3, ujumbe mpya wa Umoja wa Mataifa wa kuisaidia Somalia, UNSOM, utaanza majukumu yake, ambayo ni tofauti na yale yalotekelezwa na UNPOS. Katika taarifa ilotolewa leo, UNPOS imetoa shukrani kwa mchango wa wote walosaidia [...]

02/06/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mizozo Afrika imepungua lakini kuna vitisho vipya vya amani na utulivu:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Kusongesha mbele harakati za maendeleo kama msingi wa amani ni kauli ambazo nimetoa wakati nilipotembelea Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC nikiambatana na Rais wa benki ya dunia, ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon wakati wa mjadala wa wazi kuhusu amani na utulivu kwenye kongamano la tano la Tokyo [...]

02/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufanisi wa kudhibiti malaria wahitaji juhudi za kitaifa na ufadhili

Kusikiliza / Ugawaji wa vyandarua nchini Senegal

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameliambia kongamano la tano la kimataifa la Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika, TICAD kuwa ugonjwa wa malaria ni janga la kibinadamu ambalo huzipokonya familia watoto wao na kuzihuzunisha jamii, na hivyo ufanisi katika vita dhidi ya ugonjwa huo utahitaji nchi kuuvalia njuga na pia misaada inayotumika vyema. [...]

02/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aitaka serikali ya Sudan Kusini kujizatiti kuwalinda raia

Kusikiliza / Wakazi wa Jonglei waliokimbia vurugu

Katika mikutano yake ya ana kwa ana na viongozi wa Afrika mjini Yokohama, Japan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa Sudan Kusini, Salva kiir Mayardit. Viongozi hao wawili wamezungumza kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya Septemba 27 2012 yalosainiwa kati ya Sudan na Sudan Kusini kuhusu masuala [...]

02/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban na Kikwete wajadili albino na mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, mjini Yokohama, Japan.  Viongozi hao wawili wamezungumza kuhusu hali nchini Madagascar na pia kuhusu haja ya nchi za Afrika kuongea kwa sauti moja kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi.  Mbali [...]

02/06/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Amos/Pillay wataka raia waruhusiwe kutoka kwa usalama Al-Qusayr inSyria.

Kusikiliza / Syria

Mratibu mkuu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos na kamishina Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay wameelezea kusikitishwa kwao na ripoti kwamba maelfu ya raia wamekwama wakati mapigano makali yakiuzingira mji wa Al-Qusayr nchini Syria. Katik taarifayaoJumamosi maafisa hao wamesema wanatambua kunaweza kuwa na watu takriban 1500 waliojeruhiwa ambao wanahitaji kuhamishwa kwa ajili [...]

02/06/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031