Tuna hofu watu wanazuiwa kuondoka Syria: UNHCR

Kusikiliza /

 

Wakimbizi kutoka Syria

Wakati ghasia zinapoendelea kushamiri nchini Syria shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa watu zaidi wataendelea kutafuta usalama na misaada nje ya mipaka ya nchi hiyo. Jason Nyakundi na ripoti zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

UNHCR inasema imetiwa wasiwasi na ripoti kuwa wasyria wanaokimbia ghasia huenda wamekwama kweneye mpaka katika maneneo ambayo ni hatari. UNHCR pia inasema kuwa inasumbuliwa na madai kuwa kuna vizuizi dhidi ya wale walio na nia ya kuihama Syria . Melisa Fleming kutoka UNHCR anaeleza.

(CLIP YA MELISA FLEMING)

UNHCR inasema kuwa kwa siku saba mfululizo hakuna dalili za kuwasili kwa watu kwenye kambi ya Zaatari. Jordan inasema mipaka yake imefunguliwa. Awali hadi watu 2000 walikuwa wakivuka na kuingia nchini Jordan kila siku.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031