Wataalamu kwenye Umoja wa Mataifa wataka haki za wanaobaguliwa kulindwa

Kusikiliza /

Watu waliotengwa walindwe

Wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, wamesema ubaguzi utokanao na mfumo wa matabaka bado umeenea na kukita mizizi, huku waathirika wakikumbana na kutengwa kimfumo na kunyanyapaliwa, lakini wanaotekeleza uovu huo hawawajibishwi kisheria kwa kiwango kikubwa.

Wataalam hao wametoa wito kwa serikali kote duniani ziimarishe ulinzi wa zaidi ya watu milioni 260 ambao wanaathiriwa na ubaguzi unaoambatana na kazi wanazofanya au asili yao- wakiitwa wasoweza kujumuika na matabaka mengine, au 'untouchables'.

Wataalam hao wamesema ubaguzi wa aina hiyo huhusisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ukiwemo ukatili, wakitoa mfano wa wanawake na wasichana wa Dalit nchini Nepal, ambao wanaishi katika hatari ya kuuzwa na kudhulumiwa hata kingono kwa sababu ya jinsia na kuchukuliwa kuwa wa tabaka la chini.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031