Wanaowadhulumu wanawake Bangladesh wawajibishwe: Mtaalam wa UM

Kusikiliza /

Rashida Manjoo

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhuluma dhidi ya wanawake, Rashida Manjoo, ametoa wito kwa serikali ya Bangladesh ishughulikie changamoto wanazokumbana nazo wanawake walokumbana na ukatili wakati wakitafuta kutendewa haki. Alice kariuki na taarifa zaidi:

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Kutotekeleza sheria zilizopo na kutokuwepo mifumo ya sheria inayoitikia malalamishi na kutowawajibisha wanaotenda ukatili dhidi ya wanawake ni jambo la kawaida nchini Bangladesh, amsema Bi Rashida Manjoo, baada ya kukamilisha ziara yake ya siku kumi nchini humo mnamo Mei 29.

Mtaalam huyo kuhusu dhuluma dhidi ya wanawake amesema dhuluma zilizoenea zaidi dhidi ya wanawake ni ukatili wa nyumbani, huku asilimia kubwa ya wanawake wakiripoti kudhulumiwa na waume zao au ndugu za waume zao.

Aina nyingine za dhuluma zilizopo ni zile za kingono, zikiwemo ubakaji, ubaguzi na dhuluma kwa misingi ya kikabila, dini, tabaka, asilia, ulemavu, ndoa za utotoni na za kulazimishwa pamoja na kunyanyaswa kiuchumi, ikiwemo usafirishaji haramu.

Bi Manjoo ametaka wanawake wapewe uwezo pamoja na kuwepo mabadiliko ya kijamii ili kukabiliana na sababu za kimfumo za ubaguzi na kuongeza uwajibikaji kisheria kwa wale wanaowatendea wanawake ukatili

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031