Visa vipya vya maambukizi ya virusi vya corona vyanainika Saudia:WHO

Kusikiliza /

Wizara ya afya ya Saudia imeliarifu shirika la afya duniani WHO kwamba kumekuwa na visa vipya vilivyothibitishwa maabara vya maambukizi ya virusi vya Novel Corona.

Pia serikali hiyo imesema wagonjwa wawili walioathirika na virusi hivyo wamefariki dunia Ijumaa iliyopita huku mmoja akisalia katika hali mahtuti hospital. Kwa mujibu wa WHO uchunguzi unaendelea ambao unahusisha mlipuko wa maradhi hayo yanayoathiri mfumo wa hewa na kuhusisha majengo ya hospitali.

Hadi sasa watu 17 wamethibitishwa kuambukizwa vitusi hivyo na saba wameaga dunia. Miongoni mwa waliokufa 10 ni wanaume na watatu ni wanaa umri wa kati ya miaka 24 hadi 95. Na wakati uchunguzi ukiendelea WHO imetoa wito wa watu kuwa makini na matatizo yoyote ya kupumua lazima yachunguzwe kwa kina.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031