Vifo nchini Iraq vimeongezeka saana tangu 2008:UNAMI

Kusikiliza /

 

Baghdad

Takwimu za vifo zilizotolewa leo na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI zinaonyesha kwamba mwezi wa April mwaka huu vimeshuhudiwa vifo vingi zaidi tangi Juni mwa ka 2008. Jumla ya watu 712 wameuawa na wengine 1633 kujeruhiwa katika vitendo vya kigaidi na machafuko mengine.

Idadi ya raia waliouawa kwa mwezi April ni 595 wakiwemo polisi 161 wa kiraia, huku wale waliojeruhiwa ikifikia 1438 na polisi wa kiraia 290. Kwa upande wa majeshi 117 wameuawa na kuwaacha wengine 195 wakijeruhiwa vibaya.

Mji mkuu Baghdad ndio ulioathirika zaidi na vifo hivyo ambako raia 697 wameuawa na na majeruhi 486 , ukifuatia na mji wa Diyala, Salahuddin, Kirkuk, Ninewa na Anbar.

UNAMI imesema inafanya uchunguzi wa athari za vita vya siala kwa raia. Takwimu hizo za vifo kwa mujibu wa UNAMI huenda zikawa ni ndogo kuliko hali halisi kutokana na sababu mbalimbali.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930