Kukata na kula moyo wa maiti Syria ni uhalifu ulokithiri: Pillay

Kusikiliza /

 

 

 

Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay, amesema video kutoka Syria inayoonyesha kiongozi wa waasi akikata na kuula moyo wa mwanajeshi wa serikali inabainisha kitendo cha uovu wa kupindukia.

Bi Pillay amesema kukatakata maiti wakati wa vita ni uhalifu wa kivita, na kuongeza kuwa ingawa bado ni vigumu kuthibitisha video hiyo, makundi ya wapiganaji wa upinzani nchini Syria yanatakiwa yafanye kila yawezayo kukomesha uhalifu kama huo wa kinyama.  

Ameyataka makundi hayo kufanya uchunguzi kuhusu tukio hili na mengine ya ukiukwaji mbaya zaidi, ukiwemo vitendo vya kutesa na mauaji ya mateka wa vita.

Amerejelea wito wake wa kuliomba Baraza la Usalama liipeleke kesi ya Syria kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC, ili watu wanaoaminika kuwajibika kwa uhalifu mbaya zaidi wa kimataifa, ukiwemo uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, wakabiliwe kisheria, bila kujali wapo upande wa serikali au upinzani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2016
T N T K J M P
« apr    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031