Uzalishaji wa nafaka watarajiwa kuongezeka mwaka 2013

Kusikiliza /

Uzalishaji wa juu wa nafaka ikiwemo ngano, mchele na mahindi unatarajiwa kuongezeka duniani mwaka 2013 kulingana na utabiri uliochapishwa mwezi huu na Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linasema kuwa zao la ngano duniani mwaka 2013 linatarajiwa kufika tani milioni 695 ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.4 kutoka mwaka uliopita. FAO inasema kuwa mazao ya nafaka yanatarajiwa kundikisha rekodi mpya kwa zaidi ya tani 1,266 yakiwa ni ya juu kwa asilimia 9.3 ikilinganishwa na ya mwaka 2011. Kati ya mazao hayo mahindi yanatarajiwa kuandikisha jumla ya tani 960 ikiwa ni ongezeko la asilimia 10 kutoka mwaka 2012. Ongezeko la juu zaidi linatarajiwa nchini Marekani ambayo ndiye mzalishaji mkubwa zaidi duniani ambapo mazoa yanatarajiwa kuwa ya juu zaidi tangu mwaka 1936. FAO pia inatarajia kuongezeka kwa mazao ya mchele mwaka 2013 hadi tani milioni 500 ambapo uzalishaji wa juu unatarajiwa kushuhudiwa nchini India na Indonesia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930