Usalama huko Pibor, Kusini Sudan wazidi kuzorota: UNMISS

Kusikiliza /

Wakazi wa eneo la Pibor

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake juu ya kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama kwenye mji wa Pibor na viunga vyake huko huko jimbo la Jonglei Sudan Kusini. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS umetaja vitendo kama vile uporaji kama wa vyakula, ghasia na watu kukimbia makazi yao kuwa ni mambo yanayozoresha usalama na kutaka serikali ihakikishe watuhumiwa wanakabiliwa na mkono wa sheria. UNMISS imesema ina hofu zaidi kutokana na uvumi kuwa baadhi ya askari wasio na nidhamu na wengine walioasi jeshi wanadaiwa kuhusika na vitendo hivyo huku kikundi chenye silaha kinachoongozwa na David Yau Yau kikitaka raia kuondoa mji wa Pibor na ule wa Kapoeta ulioko jimbo la mashariki la Equitoria. Msemaji wa UNMISS Ariane Quentier amesema wanataka serikali ichukue hatua na kwamba serikali hiyo hiyo ina wajibu wa kulinda raia wake.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031