UNFPA yazindua mipango ya kuboresha afya ya uzazi

Kusikiliza /

 

Mama na wanawe

Shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA litazindua mipango mipya miwili kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango na kuboresha afya ya wajawazito kwenye maeneo ambayo ni magumu zaidi kufikika duniani. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (Taarifa ya Grace )

 Miradi  hii inaunganisha jitihada za UNFPA za zaidi ya miaka 40 za kuunga mkono upangaji jamii na kuonyesha uongozi wake katika kubuni njia mpya za kuwahami watu walio mstari wa mbele kuwafikia watu waliotengwa katika jamii. Watu hao watatangazwa kwenye kongamano la wanawake litakalofanyika mnamo mei 28-30 ,Kuala Lumpar,Malaysia.

 Mei 30 UNFPA itatangaza mradi mpya kwa ushirikiano na Shrikisho la upangaji uzazi wa kimataifa (IPPF)kwa ajili ya kulenga maswala ya jamii ya watu waliotengwa na wale walioko kwenye mazingira ya mizozo na walioko kwenye mazingira ya mabadiliko.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la idadi ya watu la Umoja wa Matiafa Dkt. Babatunde Osotimehin ambaye atajumuika na wanawake wengine wanaotambulika katika kongamanohiloamesema kwamba haitoshi tu kugawa vifaa vya uzazi wa mpango bali wanaangalia suala hili kwa ujumla.

Mradi huu unanuia kuhamasisha jamii kujitolea kwa hiari katika juhudi za kupanga uzazi na pia unalenga vijana na watu waliotengwa katika jamii.

UNFPA na IPPF watajumuisha serikali za matifa yale yaliyo na mifumo ya chini ya upangaji uzazi kama vileBolivia, Côte d’Ivoire, Ethiopia, Haiti, India, Myanmar, South Sudan na nchi nyinginezo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031