Umoja wa Mataifa kuanzisha kambi mpya ya wakimbizi wa Syria huko Jordan

Kusikiliza /

UM kufungua kambi mpya kwa ajili ya wahamiaji wasyria

Umoja wa Mataifa umetoa takribani dola Milioni Kumi kwa ajili ya uanzishwaji wa kambi mpya ya wakimbizi wa Syria huko Jordani. Maelezo zaidi na George Njogopa. (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kambi hiyo mpya inatazamiwa kuwekwa katika mji wa Azraq ulioko umbali wa kilometa 100 mashariki mwa mji mkuu wa Jordan Amman.

Inatazamia kuchukua jumla ya wakimbizi wapatao 110,000 ifikapo mwishoni mwa mwaka  na kukamilika kwake itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza hali ngumu inayoandama kambi ya Za'atari ambayo hadi sasa imeshapokea wakimbizi zaidi 100,000.

Fedha za kukamilishwa kwa kambi hiyo zinatazamiwa kuratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na lile la kuhudumia watoto UNICEF ambayo yote kwa pamoja yamelenga kuwasaidia zaidi ya wakimbizi 50,000 ambao wapo kwenye mazingira magumu.

Serikali ya Jordan inasema kuwa zaidi ya raia 500,000 wa Syria wanaishi maisha ya ukimbizi nchini humo tangu kuzuka kwa mapigano Marchi mwaka 2011.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031