Ulimwengi unahitaji wakunga zaidi:UNFPA

Kusikiliza /

Ulimmwengu unahitaji wakunga zaidi,UNFPA, picha/UNFPA

Wakati ya kujifungua kwa mama kunatajwa kuwa kupindi  kilicho hatari zaidi na cha miujiza  kwa maisha ya mwanamke.

Wakunga wamechukua wajibu mkubwa katika jitihada za kupunguza hatari zinaowakumba wanawake wanapojifungua. Wakiwa na ujuzi wa juu, wakunga sasa wanaweza kukubiliana na  hatari zinaowakumba akina mama na wana wajibu mkubwa wa kuyaweka maisha  ya mama kuwa salama kote duniani.

Wakunga huwauguza akina mama kabla na baada ya kujifungua, wanalinda afya za watoto wanaozaliwa , wanatoa ushauri kuhusu upangaji uzazi, wanazuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na wanafahamu wakati wa kuitisha huduma za dharura.

Inakadiriwa kuwa wakunga walio na mafunzo na wanaopata msaada wanaweza kuokoa  maisha ya zaidi ya wanawake 200,000 kila mwaka na mara kumi zaidi ya watoto kiasi hicho.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2015
T N T K J M P
« nov    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031