Uhamishwaji wa familia ya Kibedui ulikiuka sheria za Kimataifa- Utafiti

Kusikiliza /

Utafiti mpya ambao ni wa aina yake uliomulika hatua ya kuhamishwa bila hiari kwa wakimbizi 150 wa Kipalestina toka familia za kibedui kulikofanywa na utawala wa Israel umeonyesha kuwa familia hizo haziridhika na hali hiyo na kwamba sehemu waliyopelekwa haina tija kijamii wala kiuchumi.

Katika ripoti yao ya pamoja iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA na taasisi ya Bimkom,iliyoendesha utafiti huo imeonyesha kwamba zoezi la kuwahamisha wakimbizi hao lililoanza kutekelezwa mwaka 1997 ili kupisha upanuzi wa makazi Ma'ale lilikuwa kinyume na sheria za kimataifa.

Utafiti huo umebanisha kuwa familia hiyo ya Kibedui ambayo ilihamishiwa katika kijiji cha Al Jabal haijaridhishwa na hatua hiyo .

Kama ilivyonukuliwa na ripoti hiyo mpya, familia hiyo imesema kuwa kitendo hicho cha kuwahamisha kinguvu kimevuruga utamaduni wao wa asili hat utambulisho wao umedhihakiwa na kuporomoshwa vibaya.

Kwa mujibu wa Msemaji wa UNRWA , Chris Gunness, amesema kuwa mamlaka ya Israel inafikiria kuanzishwa makazi mengine kwa ajili ya kuwahamishia familia ya Kibedui inayoendelea kuishi kwenye Ukingo wa Ukanda wa Gaza.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2016
T N T K J M P
« ago    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930