TEKNOHAMA yabadili mfumo wa biashara kwa wajasiriamali wanawake

Kusikiliza /

ujasiriamali na teknolojia

Mkutano wa kimataifa wa Jamii Habari wa tarehe 13 hadi 17 Mei huko Geneva, Uswisi ulioandaliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la mawasiliano, ITU pamoja na mambo mengine unaangalia fursa mpya kwa wajasiriamali wanawake za kuimarisha biashara zao kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano, TEKNOHAMA au ICT kwa kimombo. Mathalani matumizi ya simu za mkononi, mitandao ya kijamii na kadhalika. Patrick Maigua wa Radio ya Umoja wa Mataifa huko Geneva, amefanya mahojiano maalum na mshiriki kutoka Tanzania kwenye mkutano huo Blandina Sambu kuweza kufahamu jinsi TEKNOHAMA inavyosaidia na wigo wake katika kufikia pia wanawake wa vijijini. Hapa Blandina anaanza kwa kuangalia wanawake walikotoka na biashara.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2016
T N T K J M P
« jun    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031