Siku ya Vesak siyo kwa mabudha tu: Ban

Kusikiliza /

Sherehe za siku ya Vesak

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Vesak ambayo ni sherehe maalumu kwa ajili ya Mabudha kote duniani ni fursa nzuri pia kwa jumuiya ya kimataifa kufaidika na utajiri wa utamaduni wa Kibudha. Katika taarifa yake amesema maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika wakati kukiwa na machafuko na mikasa mingi duniani na ni wakati muafaka wa kuangalia jinsi maadili ya Kibudha yanavyoweza kusaidia kukabiliana na changamoto akisema kuwa kukabili changamoto za dunia vina mashabihiano na Ubudha.  Akitoa mfano wa Budha mwenyewe aliyekuwa mwanamfalme aliacha kasrilakenakwenda kutanabahi machungu manne yanayomkabili mwanadamu ambao ni kuzaliwa, maradhi, uzee na kifo. Amesema wakati machungu hayo hayaepukiki Ubudha unatoa mwangaza wa jinsi gani ya kukabiliana na mambo hayo na ni historia inayoambatana na uwezo mkubwa wa falsafa ya Kibudha. Akiwatakia kila la heri Mabudha wote duniani katika siku ya Vesak, Ban amesema dunia hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote  inahitaji mtazamo usio na hila ya machafuko ili kusaidia kuchagiza amani na kuepuka vita, na anatumai wote watahamasishwa na mtazamo wa Kibudha katika kuifanya dunia kuwa mahala salama pa kuishi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2016
T N T K J M P
« apr    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031