Siku ya Albino Tanzania leo: UM wataka hatua zaidi zichukuliwe kuwalinda

Kusikiliza /

watoto albino nchini Tanzania

Nchini Tanzania leo ni siku ya kitaifa ya Albino ambapo jopo la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka mamlaka zote husika kuzuia mauaji ya Albino na uchunguzi wa kina ufanyike dhidi ya watekelezaji wa vitendo hivyo.  Mmoja wa wataalamu hao Juan E Mendez amesema utekelezaji wa vitendo vyovyote vya kikatili hauwezi kuhalalishwa na kwa mujibu wa sheria za kimataifa ni jukumu la serikali kuwapatia albino ulinzi dhidi ya wale wanaotaka kuwakatili. Ametoa kauli hiyo kutokana na kuwepo kwa taarifa za mauaji ya Albino na viungo vyao kutumiwa kwa imani potofu za kishirikina nchini Tanzania na katika baadhi ya nchi barani Afrika. Naye Kishore Singh ambaye amejikita katika  hali ya elimu amesema kuwepo kwa siku ya kitaifa nchini Tanzania ni fursa kubwa ya kumulika tatizo hilo na kuibua mjadala wa madhila yanayowakumba albino nchini humo. Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania, LHRC hushiriki kuelimisha watu juu ya haki za binadamu ikiwemo ulinzi wa Albino, nimezungumza na Kaimu Mkurugenzi wake Harold Sungusia kufahamu hali iko vipi hivi sasa?

 (SAUTI HAROLD)

 Na nini basi kifanyike ili kudhibiti hali hiyo?

 (SAUTI-HAROLD)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930