Mzozo Afrika ya Kati una madhara makubwa ukanda mzima: Ripoti

Kusikiliza /

Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepokea ripoti ya katibu Mkuu kuhusu utendaji wa ofisi ya umoja huo kwenye ukanda wa Afrika ya Kati na maeneo yanayoathiriwa na kikundi cha Lord's Resistance Army ambayo inaeleza kuwa mzozo Jamhuri ya Afrika ya Kati umekuwa na madhara makubwa katika harakati za kudhibiti vitendo vya kikundi cha waasi cha Lord's Resistance Army, LRA na kujenga amani ya kikanda.

Mkuu wa ofisi yaUmoja wa Mataifa kwenye ukanda huo, UNOCA, Abu Mousa akisoma ripoti hiyo amesema mgogoro huo umesababisha kusambaaa kwa silaha kwenye eneo hilo na hata kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati kuelekea nchi jirani.

Ripoti imependekeza hatua kadhaa ikiwemo kurejesha haraka kwa amani na utulivu Jamhuri ya Afrika ya Kati kama njia mojawapo ya kuleta amani ukanda wa Afrika ya Kati.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031