MONUSCO yapata Kamanda mpya, ni Carlos Alberto Dos Santos Cruz

Kusikiliza /

Lt. jenerali Carlos Alberto Dos Santos Cruz

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteua Luteni Jenerali Carlos Alberto Dos Santos Cruz wa Brazil kuwa Kamanda Mkuu wa ujumbe wa Umoja huo unaoweka utulivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, MONUSCO.Anaziba nafasi iliyoachwa na Luteni Jenerali Chander Prakash Wadhwa wa India, aliyemaliza kipindi cha uhudumu tarehe 31 mwezi Machi mwaka huu ambaye pia Bwana Ban amemsifu kwa kile alichosema uongozi wa kujitoa wa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

Luteni Jenerali Santos Cruz ameelezwa kuwa na uzoefu wa miaka 40 wa kitaifa na kimataifa katika masuala ya kijeshi ambapo kabla ya uteuzi huu alikuwa mshauri maalum wa waziri kwenye ofisi ya Rais wa Brazil.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29