Mkuu wa UNHCR azitaka nchi kuheshimu sheria za kimataifa baada ya Mkorea kutimuliwa Laos

Kusikiliza /

António Guterres, UNHCR

Kamishina mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR Bwana Antonio Guterres ameelezea hofu yake leo dhidi ya ulinzi na usalama wa Wakorea tisa ambao wameripotiwa kutimuliwa kutoka nchiniLaosna kupelekwaChina.Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na UNHCR kundi la watu hao tisa wakiwemo watoto watano walikamatwa Jamuhuri ya Laos Mai 10 na kuondolewa kwa nguvu kupelekwa Uchina Mai 27.

UNHCR inahofia kwamba watu hao waliotimuliwa hawakuwa na fursa ya madai yao ya ukimbizi kusikilizwa na kutathiminiwa.

Bwana Guterres ameyataka mataifa yote duniani kuzingatia misingi ya ulinzi dhidi ya kushitakiwakamakigezo katika kufuata sheria za kimataifa na kujizuia kuchukua hatua zozote katika siku za usoni ambazo zitasbabisha watu kurejea kwenye nchi ambazo maisha au uhuru wao uko hatarini.

Pia ameitaka serikali yaLaoskutoa sababu za tukiohilona kuhakikisha inazuia kufanyika tena kitendo kama hicho.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031