Mipaka isopodhibitiwa huchangia ugaidi:Ban

Kusikiliza /

 

kupambana na ugaidi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema ugaidi hunawiri pale udhibiti wa mipaka unapokuwa hafifu. Bwana Ban amesema ili kuhakikisha kuwa ugaidi unakabiliwa ipasavyo, nchi na kanda zinazoathiriwa zinatakiwa kusaidiwa kuimarisha uwezo wao wa mifumo ya usalama.

Katibu Mkuu amesema hayo wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu amani na usalama barani Afrika, ambao pia umeangazia masuala ya ugaidi na ulanguzi wa fedha

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

''Kutokuwepo maendeleo na uongozi wa kisheria huruhusu makundi ya kigaidi kuwavuta watu kutoka jamii zote na kuongeza ufuasi. Uhusiano baina ya magaidi ya makundi ya uhalifu wa kimataifa wa kupangwa unasaidia kuendeleza usafirishaji wa watu, fedha, silaha na bidhaa haramu kuvuka mipaka, na kuchangia ueneaji na uendelezaji wa makundi haya. Katika mazingira kama hayo, jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa ni lazima kuongeza juhudi za kuimarisha uwezo wa nchi wanachama zilizoathiriwa'' 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031