Mauaji ya raia kaskazini mwa Nigeria ni lazima yachunguzwe: UM

Kusikiliza /

 

Msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Rupert Colville

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kutaka kufanyika kwa uchunguzi ulio huru kuhusu mauaji ya karibu watu 200 kaskazini mwa Nigeria wakati wa oparesheni moja ya kuwavurusha wanamgambo wa kislamu. Alice Kariuki na ripoti kamili.

(PKG YA ALICE KARIUKI)

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa oparesheni hiyo iliyoendeshwa kwenye mji wa Baga jimbo la Borno ilisababisha vifo vya raia wengi, ikasababisha uharibifu mkubwa wa nyumba na mali na kuhama kwa watu. Zaidi ya nyumba 200 ziliharibiwa wakati wa oparesheni hyo iliyoendeshwa kufuatia kuuawa kwa mwanajeshi mmoja na wanamgambo wa kundi la Boko Haram. Pillay anasema kuwa jeshi na maafisa wengine wa usalama ni lazima waheshimu haki za binadamu na kuzuia matumizi wa nguvu kupita kiasi wakati wanapoendesha oparesheni kama hizo. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Kundi la Boko Haram limekuwa likihusika kwenye misururu ya utekaji nyara , mauaji ya raia na wanasiasa, maafisa wa usalama na raia wa kigeni.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031