Marekani iheshimu maisha na haki za wafungwa Guantanamo:UM

Kusikiliza /

Rupert Colville

Marekani ni lazima iheshimu na kuwahakikisha maisha, afya na hadhi ya wafungwa wanaoshikiliwa kwenye kituo cha Guantanamo hususani katika hali inayoendelea sasa ya mgomo wa kula.

Hayo yamesemwa na kundi la wataalamu wa kimataifa wa haki za binadamu kuhusu masuala ya utesaji, mahabusu, vita dhidi ya ugaidi na afya.

Wataalamu hao wanasema wamepokea taarifa kuhusu athari za kiafya na kiakili kwa wafungwa kufuatia sintofahamu ya hatima yao, kwa mfano kutojua endapo wafikishwa mahakamani au wataachiliwa na lini, au kama wataziona familia zao tena.

 

Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa akifafanua kuhusu mgomo wa kula na mustakhbali wa kituo cha Guantanamo

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2016
T N T K J M P
« ago    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930