Mamilioni wakabiliwa na hali mbovu ya kibinadamu Yemen:OCHA

Kusikiliza /

Mkuu wa Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed, amesema nchi hiyo inakabiliwa na kuzorota zaidi kwa hali ya kibinadamu, ambayo huenda ikasababisha hali tete ya kisiasa iliyopo sasa nchini humo kutumbukia matatani. George Njogopa anaripoti

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Kulingana na mratibu Cheikh Ahmed, kiasi cha watu milioni 10 wapo katika hali ngumu wakihitaji misaada ya chakula na watu milioni 5 kati ya hao wapo katika hali mbaya zaidi.

Kuna watu wengine wanaokadiriwa kufikia milioni 6 wanakabiliwa na tatizo la kutofikiwa na huduma za afya na wakati huo huo kunaelezwa kwamba kiasi cha watoto milioni moja wanamatatizo ya utapiamlo.

Kati ya watoto hao 100,000 wapo hatarini kupoteza maisha kutokana na hali zao kuwa mbaya zaidi.

Taifa hilo pia linaandamwa na matatizo mengine ikiwemo la watu zaidi ya 340,000 ambao hawana makazi maalumu kutoka na mapigano yaliyozuka katika eneo la kaskazini ambako nyumba kadhaa ziliharibiwa.

(SAUTI YA SHEIK AHMED)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930