Wakimbizi wa Mali kushiriki katika uchaguzi ujao kutoka nchi jirani

Kusikiliza /

Zaidi ya watu 174,000 raia wa Mali, ambao wamekimbilia nchi jirani watawezeshwa kushiriki katika uchaguzi ujao wa urais kwa msaada wa Shirika la Unoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi, UNHCR.

George Njogopa anaripoti

 

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA

Kumekuwa na majadiliano yanayoendelea baina ya serikali ya Mali na nchi ambazo zinahifadhi wakimbizi hao ili kuwawezesha wakimbizi hao kushiriki kwenye uchaguzi ujao.

Tangu kuzuka kwa mzozo huo wa Mali, zaidi ya raia 50,000 wanaripotiwa kuingia nchi jirani ya Burkina Faso na kuomba ukimbizi, wakati wengine wapatao 74,000 wako nchini Mauritania. Pia wakimbizi wengi ne wanaokaridiwa kufikia 50,000 wako Niger.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa shughuli za upigaji kura zitafanywa kwa hiari ya wakimbizi wenyewe na kwamba shirika hilo litashirikiana na nchi husika kufanikisha zoezi hilo.

Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR aliyeko Geneva:

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930