Makabila ya asili yasipuuzwe, nayo huchangia maendeleo: UM

Kusikiliza /

Chifu Mkuu wa taifa lijulikanalo kama Onondaga Todadaho Sid Hill

Kikao cha kudumu cha Umoja wa Mataifa kinachojadili masuala ya makabila asili kimeanza Jumatatu mjini New York, Marekani.Kikao hicho kilianza rasmi kwa kupigwa wimbo maalum. Na baada ya taratibu zote kukamilika ikiwemo kuchaguliwa kwa Paul Kanyike Sena kutoka Kenya kuwa mwenyekiti wa kikao hicho cha 12, Rais wa Baraza la uchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, Néstor Osorio alihutubia na kusifu wingi wa wajumbe waliojitokeza kushiriki kikao hicho.

Amesema hali hiyo inadhihirisha kuimarika kwa jitihada za kuboresha maslahi ya watu wa asili maeneo mbali mbali duniani ambao katika maeneo mengi mila zao za kijadi mathalani kwenye tiba na kilimo zinapuuzwa wakati zinaweza kuboreshwa na kutumika katika maendeleo.

(SAUTI YA OSORIO)

Ametaka kikao hicho kiangalie jinsi ya faida za kazi za makabila ya asili zitakuwa na manufaa kwao pia badala ya kunufaisha wachache kwa kuwa makabila asili nayo yana nafasi kubwa katika maendeleo ya nchi na dunia nzima.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031