Maisha ya watembea kwa miguu yakatiliwa kwa ajali barabarani -WHO

Kusikiliza /

Ripoti ya Shirika la afya duniani, WHO inaonyesha kuwa watembea kwa miguu zaidi ya 5000 hufa kila wiki kwa ajali za barabarani kutokana na umuhimu wao kutozingatiwa.Joseph Msami na maelezo zaidi

(RIPOTI YA JOSEPH MSAMI)

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, na afya ya akili wa WHO Etenne Krug, utafiti huo ambao unakuja wakati wa maadhimisho ya pili ya kimataifa ya usalama barabarani unaonyesha kuwa barani Afrika vifo vya watembea kwa miguu ni asilimia 38, ukanda wa kusini mwa Asia ailimia 12, wakati nchini El Salvador ,kusini mwa Amerika vifo vya watembea kwa miguu ni takribani theluthi mbili ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani nako nchini Liberia vifo hivyo ni asilimia 66.

Kwa mujibu wa utafiti huo wa WHO, katika nchi zenye kipato kidogo na cha kati wanaoathirika zaidi ni vijana na watoto wakati katika nchi zilizoendelea walioko katika hatari zaidi ni wazee.

(SAUTI YA KRUG)

Kauli mbiu ya maadhimisho ya kimataifa ya usalama barabarani Mei sita hadi kumi na mbili ni kuwahakikishia watembea kwa miguu usalama.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930