Madhila yanayosababishwa na binadamu DRC sasa yakome: Kyung-Wha

Kusikiliza /

Madhila yanayosababishwa na binadamu DRC sasa yakome: Kyung-Wha
Kyung-Wha Kang

Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA Kyung-Wha Kang amekutana na wakimbizi wa ndani huko Sotraki karibu na mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Goma huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na kusema kuwa mateso yanayosababishwa na binadamu yanapaswa kukoma. Bi. Kyung-Wha alifika eneo hilo linalohifadhi takribani wakimbizi Elfu Tatu wa ndani tangu kuibuka upya kwa mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi wa kikundi cha M23 wiki iliyopita. Amesema mauaji ya raia kutokana na mashambulizi ya wiki iliyopita hayakubaliki na ametaka pande zote husika kwenye mapigano hayo kuheshimua sheria za kimataifa kuhusu binadamu. Amesema sasa wakati umefika wa kumaliza dharura hiyo ya kutisha inayosababishwa na binadamu. Akiwa hapo Sotraki katika siku yake ya pili ya ziara ya siku nne aliyoanza Jumatatu huko DRC Bi, Kyung-Wha ameshuhudia kazi za mashirika yasiyo ya kiserikali na yale ya Umoja wa Mataifa na wadau wake ya kuwapatia misaada ya dharura wakimbizi wa ndani. Amesema safari ya kupata amani ya kudumu ni ndefu lakini kuna matumaini na ujasiri.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031