Kupiga marufuku matangazo ya tumbaku kunaokoa maisha: Ban

Kusikiliza /

Madhara ya uvutaji tumbaku

Leo ni siku ya kimataifa ya kupiga vita matumizi ya tumbaku duniani, ujumbe mkuu ni kwamba serikali zipige marufuku matangazo ya biashara ya bidhaa za tumbaku ikiwemo sigara ili kuokoa maisha ya binadamu. Taarifa ya Assumpta Massoi inaarifu zaidi.

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Katika kuadhimisha siku ya kupiga marufuku matumizi ya bidhaa zote za tumbaku duniani hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe na kusema matumizi ya bidhaa za tumbaku ikiwemo sigara ni moja ya tishio kubwa kwa afya ya binadamu kwa kuwa nusu ya watumiaji hufariki dunia.

Amesema iwapo dunia inaweza kupunguza fursa ya watu kukumbana na matangazo yanayochochea uvutaji tumbaku basi inaweza kupunguza idadi mpya watumiaji wapya.

Amezisihi nchi duniani kutekeleza mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya tumbaku wa WHO unaopiga  marufuku matangazo ya biashara ya bidhaa za tumbaku. Glen Thomas ni msemaji wa WHO.

(SAUTI YA GLEN THOMAS)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031