Kongamano kuhusu majanga duniani laanza Geneva kwa pole kwa wahanga wa janga la tufani Oklahoma

Kusikiliza /

Baada ya tufani iliyoikumba Oklahoma

Kongamano la umoja wa Mataifa lenye lengo la kuzihakikishia jamii usalama kutokana na majanga  limengo'a nanga hii leo mjini Geneva Uswisi likionyesha huzuni yake kwa watu wa mji wa Oklahoma,  uharibifu na kupotea kwa maisha kutokana na janga la tufani  iliyoshuhudiwa siku Jumanne.Tufani hiyo ambayo ni moja ya tufani nyingi zilizizoshuhudiwa siku chache zilizopita magahribu mwa Marekani iliharibu shule na kusababisha vifo vingi vikiwemo vya watoto wa shule 20.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ameelezea huzuni yake kufuatia janga hilo ambapo ametuma rambi rambi zake kwa wale waliowapoteza wapendwa wao na kwa wale walioathiriwa na tufani hiyo.

Kupitia taarifa kutoka kwa msemaji wake Ban amemuandikia Gavana wa jimbo la Oklahoma Mary Fallin ambapo ametangaaza msaada kutoka kwa Umoja wa Mataifa ikiwa utaombwa kufanya hivyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031