Kiwango cha joto duniani mwaka jana kilizidi kuongezeka

Kusikiliza /

Mwaka wa 2012 ulikuwa na viwango vy joto vya juu

Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa, WMO limetoa ripoti yake kuhusu mwenendo wa hali ya duniani na kueleza kuwa mwaka 2012 umeingia katika orodha ya miaka yenye viwango vya juu zaidi vya joto licha ya athari za mkondo baridi wa baharini, La Nina.

WMO inasema mwaka 2012 wastani wa kiwango cha joto cha baharini na ardhini kilikadiriwa kuwa nyuzi joto Sufuri nukta Nne Tano zaidi ya kiwango cha nyuzi joto Kumi na Nne nukta Sufuri cha kati ya mwaka 1961 na 1990. Kiwango hicho ni cha juu na kinauweka mwaka huu nafasi ya Tisa tangu viwango hivyo vianze kunukuliwa mwaka 1850.

WMO imesema viwango hivyo vinatia hofu kwa kuwa vinachangia pia kuyeyuka kwa barafu katika bahari ya Arctic na kuongeza viwango vya maji ya bahari.

Omar Baddour ni afisa kutoka WMO na hapa anafafanua zaidi.

(SAUTI YA OMAR)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031