Kipaji cha muziki chatia matumaini miongoni mwa watoto waishio kwenye mazingira magumu Tanzania

Kusikiliza /

Watoto

Nchini Tanzania kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu,jambo ambalo linasababishwa na kukosekana kwa uthabiti kwa familia. Kundi kubwa la watoto hao wanapatikana kwa wingi katika maeneo ya miji mikubwa ikiwemo Dar es salaam, Mwanza na Arusha. Hata hivyo kumekuwa na ongezeko pia la mashairika ya kiraia ambayo yanaunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na tatizo hilo kwa kuanzisha fursa mbambali ambazo zinawapa mwanga wa matumaini vijana hao ili waweze hatimaye kuwa na maisha ya staha. Watoto wanachakarika punde wakipatiwa fursa. Je ni fursa zipi hizo? Na nini mtazamo wa maisha yao? Basi katika makala yetu leo George Njogopa kutoka Dar es salaam anaangazia juhudi zinazofanywa kuwasaidia watoto hao kupitia vipaji vyao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031