Jesús Vázquez awatembelea wakimbizi wa Syria nchini Jordan

Kusikiliza /

Jesús Vázquez

Balozi mwema wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR ambaye pia ni mtangazi maarufu wa runinga nchini uhispania Jesús Vázquez wiki ameitembelea Jordan kuangazia hali ya maelfu ya wakimbizi nchini Syria hususan watoto na kusaidia kuchangisha fedha zinazohitajika na UNHCR nchini Syria.

Akiwa kwenye kambi ya Za'atri balozi huyo amesema kuwa ziara yake ina lengo la kuwasikilika wale wanaotaabika na kusaidia kuchangisha fedha nchini mwake kukidhi mahitaji yao. Wakati wa ziara hiyo ya siku mbili nchini Jordan Vázquez pia alitembelea mji mkuu wa Amman ambapo alikutana na wakimbizi wa mijini na kujulishwa kuhusu matatizo wanayopitia. Akiwa kwenye kambi ya Za'atri ambayo inazidi kupanuka balozi huyo alikutana na wakimbizi na watoa huduma za misaada. Tangu mzozo kuanza nchini Syria machi mwaka 2011 zaidi ya watu milioni 1.4 wameikimbia Syria huku Jordan ikipokea wakimbizi 460,000.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031