Jamii ya kimataifa yaahidi dola bilioni 4.18 kukarabati Mali

Kusikiliza /

Jamii ya kimataifa kutoa msaada kwa Mali

Jamii ya kimataifa imeahidi kutoa msaada wa dola bilioni nne nukta moja, ambazo zitasaidia katika mpango wa kuiendeleza nchi ya Mali. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ALICE)

Ahadi hizo za msaada zimetolewa wakati wa mkutano uloandaliwa na serikali za Mali na Ufaransa pamoja na jumuiya ya nchi za Ulaya, mjini Brussels, Ubeljiji.

Mpango wa ukwamuaji endelevu wa Mali unanuia kurejesha udhibiti wa mipaka ya nchi hiyo na kuendeleza amani, usalama na maridhiano, pamoja na kufungua njia ya ukuaji jumuishi na maendeleo ya kudumu. Gharama nzima ya mpango huo wa ukwamuaji wa Mali ni dola za kimarekani bilioni 5.5.

Mkurugenzi Mwandamizi wa Mpango wa Maendeleo katika Umoja wa Mataifa (UNDP), Rebecca Gryspan, ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika mkutano huo, amesema mbali na kutatua matatizo ya kiusalama, utatuzi wa mzozo wa Mali pia utahitaji kukabiliana na changamoto sugu za kisiasa, kijamii na maendeleo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031