IOM yazungumzia uhusiano wa mabadiliko ya tabianchi na uhamiaji

Kusikiliza /

Nembo ya IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji limeonyesha wasiwasi wake juu ya mwelekeo wa sasa wa wahamiaji wanaotakana na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao ambapo shirika hilo limesema suala hilo linapaswa  kuwa miongoni mwa vipaumbele katika mpango wa maendeleo endelevu wa Umoja wa Mataifa baada ya ukomo wa malengo ya milenia mwaka 2015.

Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa amesema  katika karne hii na ile ijayo mabadiliko ya tabianchi yatasababisha maafa mengi na hivyo wanajamii kuhama katika meneo mbalimbali kwa ajili ya kutafuta makazi salama.

Mathalani amesema kwa miongo miwili iliyopita mabadiliko ya tabianchi yamesababisha ukame nchini Somalia na wengi wa raia wa  nchi hiyo kuhama na kuongeza kuwa IOM inafanya tahthimini ya kitaalamu juu ya athari za mabadiliko hayo  na kutoa mapendekezo kwa Umoja wa Mataifa na jumiya ya kimataifa kwa ujumla juu ya namna ya kukabiliana na athari hizo.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE )

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930